“Do not be embarrassed by your mistakes. Nothing can teach us better than our understanding of them. This is one of the best ways of self-education.” —THOMAS CARLYLE

Ni siku nyingine nzuri, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tuna nafasi hii kubwa mbele yetu ya kwenda kufanya tofauti ili kuweza kupata matokeo makubwa sana.

Kukosea ni ubinadamu, bila ya kukosea huwezi kujifunza kipi sahihi kwako kufanya.
Hivyo usione aibu kukosea, maana ni kupitia kukosea ndiyo unajifunza kilicho sahihi.

Hakuna mwalimu bora kama kukosea,
Kukosea ndiyo njia bora ya kujifunza wewe mwenyewe.
Hivyo usikimbie makosa, badala yake yakaribishe kama sehemu ya kujifunza.

Jamii yetu imetufundisha kukwepa makosa na pale yanapotokea basi kuyaficha.
Hivi ndivyo tumefundishwa tangu shuleni mpaka kwenye kazi,
Kwamba kukosea ni kubaya hivyo unapokosea unaadhibiwa.
Kwa mazingira hayo, wengi tunayaogopa sana makosa na hivyo hatufanyi mambo makubwa na ya tofauti.

Kama hukosei kwenye maisha yako, maana yake hakuna mambo makubwa na ya tofauti unayofanya.
Na hilo ni uhakika kwamba hutaweza kupiga hatua kubwa na hata kufanikiwa kwenye maisha yako.

Watson amewahi kusema kama unataka kufanikiwa zaidi, onheza makosa unayoyafanya.
Ukawe na siku ya kujaribu vitu vipya na vikubwa, ambapo utakosea na kisha kujifunza kutokaba na makosa hayo na kuwa bora zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania