“Would you like me to give you a formula for success? It’s quite simple, really. Double your rate of failure.” —THOMAS J. WATSON

Kama unataka kufanikiwa zaidi ya pale ulipo sasa, unapaswa kukosea zaidi ya ulivyokosea huko nyuma.
Kukosea ni ishara kwamba unajaribu vitu vipya na vikubwa.
Kama hukosei maana yake unafanya vitu ulivyozoea, vitu vya kawaida na hivyo lazima utapata matokeo ya kawaida.

Jua kwa hakika kile unachotaka na kisha jaribu njia mbalimbali za kukipata, baadhi ya hizo utakosea lakini pia utajifunza na kuweza kufanya kwa ubora zaidi.
Jamii itakucheka utakapokosea, lakini wewe ndiye utakayecheka zaidi utakapofanikiwa.
Kukosea kwenye makosa ni kule unakofanya bila ya kujifunza na kisha kurudia makosa yale yale.
Lakini kama unajifunza na kuwa bora zaidi, usiogope kukosea, maana hiyo ndiyo njia bora ya wewe kupiga hatua zaidi.

Kufanikiwa, kosea zaidi.
Kocha.