“The same divine beginning lives in all people, and no single person or gathering of people has the right to destroy this connection between the divine beginning and a human body, that is, to take a human life.” – Leo Tolstoy

Kupata nafasi hii nyingine nzuri ya kuiona siku hii mpya ni jambo la kipekee sana kwetu.
Tunapaswa kuitumia vyema siku hii, ili kuweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Kila maisha yana uungu ndani yake, hivyo hakuna yeyote mwenye haki ya kukatisha maisha ya wengine.
Kila mtu ni mfano wa Mungu, ukimuua mtu umemuua Mungu.
Hivyo ishi na waache wengine nao waishi.
Usijipe kazi ambayo siyo yako, wacha asili ifanye kazi yake.

Hivyo pia ndivyo inavyopaswa kuwa kwenye kazi na hata biashara zetu.
Fanya kazi yako na waache wengine wafanye kazi zao, huna haja ya kuwapikia majungu ili wafukuzwe kazi zao.
Fanya biashara yako na waache wengine wafanye biashara zao, huna haja ya kuwafanyia hila ili biashara zao zife, hata kama mnashindana.

Nani afe na nani aendelee kuishi ni maamuzi ya asili,
Biashara ipi iendelee na ipi ifungwe pia ni maamuzi ya asili,
Usiyaingilie, ni kujichosha na kujipa mizigo kwa mambo yasiyo yako.

Chukua mfano wa mbegu za miti miwili tofauti zimedondoka eneo moja, labda mwembe na mbuyu.
Hakuna mbegu itakayosema kwamba inasuburi kwanza mwenzake akue na yenyewe ndoyo ikue.
Hakuna mbugu itakayosema inabidi imuue mwenzake kwanza ndiyo yenyewe iweze kukua vizuri.
Badala yake kila mbegu inakua kivyake, kulingana ma asili yake, na baadaye, ile ambayo inatoa mmea mkubwa kuliko nyingine, inaziba yenye mmea mdogo na hivyo inakufa.
Siyo kwa kudhamiria, bali kwa asili.

Hivyo hata kama kuna mtu amekuudhi au kukukatili kiasi gani, usiingilie kazi ya asili, achana naye, iko siku hicho alichozoea kufanya kitampeleka kwenye kifo chake, usijihusishe nacho yeye.
Hata kama wengine unashindana nao kwenye kazi au biashara, acha asili iamue nani anayetoa thamani hasa na aendelee, usipoteze muda wako kuwaharibia wengine, badala yake utumie kutoa thamani zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania