Zig Zigler kwenye moja ya mafundisho yake amewahi kutoa mfano huu; iwapo adui yako mkubwa ataweka asali kwenye kikombe chako cha chai, je nini kitatolea kwako? Na je vipi kama rafiki yako mkubwa, kwa bahati mbaya akaweka sumu kwenye kikombe chako cha chai, nini kitatokea?
Kwa adui aliyeweka asali kwenye chai yako utakuwa vizuri, lakini kwa rafiki aliyeweka sumu kwenye chai yako, utakufa.
Ambacho nataka kukuambia leo rafiki yangu ni hiki, mara zote tafuta ukweli, usijali umetoka kwa nani. Kama kitu ni kweli, basi kitabaki kweli hata kama ukweli huo umepewa na mtu ambaye humpendi au humkubali.
Hii ni kwa sababu hakuna anayehodhi ukweli, ukweli ni mali ya kila mtu, ukweli haugunduliwi, bali upo na wale ambao wapo tayari kuuona basi huwa wanauona haraka.
Hivyo ni wajibu wako, kwenye kila hali kujua ukweli ni upi na kuupokea kama ulivyo na siyo kuanza kuangalia kama anayekupa ukweli huo ni mtu ambaye unakubaliana naye. Ukweli unapaswa kuwa kipaumbele chako, umetoka kwa nani hilo siyo muhimu kwako.
Kipaumbele chako kinapaswa kuwa ni kuujua ukweli, halafu ufanyie kazi ukweli huo bila ya kujali umetoka kwa nani.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Hiyo tafakari ya Maneno ya Zig ziglar bhana!!!
LikeLike
Ukweli una nguvu kubwa Sana japo una maamuzi makali Sana ,kitu muhimu kujifunza
LikeLike
Ahsante kocha, ni kweli ni muhimu kuutafuta ukweli bila kujali ukweli huo unatoka kwa nani. Na hili limenitokea leo. Kuna mtu ambaye nilipanga kukutana naye leo lakini nilipompigia simu akasema amesafiri. Sasa nikasema ngoja nikubaliane naye lakini nikaamua kujipa jukumu la kuutafuta ukweli na nikaenda hadi ofisini kwake nikamkuta yupo hadi akaona aibu.
LikeLike
Shukurani kocha , kwa hiayari yangu nitapokea ukweli bila kujua umetoka kwa nani. Siku zote za maisha yangu
LikeLike