“A wise man loves not because he wants to profit from it but because he finds bliss in love itself.” – Leo Tolstoy

Kwa mpumbavu, upendo umejishikiza na kitu, anampenda mtu kwa sababu kuna kitu anapata kutoka kwake. Upendo wa aina hii siyo sahihi na haudumu.

Kwa mwerevu, upendo haujajishikiza na chochote, anampenda mtu kwa sababu ana upendo ndani yake na kuutoa upendo huo ni sehemu ya maisha yake. Kupenda kunamfanya akamilike na hategemei kupata chochote kwa yule anayempenda.

Tunapaswa kuwa werevu kwa kuwa na upendo wa kweli, upendo usiojishikiza kwenye chochote.
Upendo una nguvu kubwa, kwa anayependa na anayependwa,
Hiyo pekee ni sababu ya kutosha kwako kuishi kwa upendo.

Uwe na usiku mwema, usiku wa kutafakari na kuianza kesho kwa upendo usiokuwa na masharti wala mategemeo ya kupata kitu fulani.
Kocha.