“No matter what anyone says or does, my task is to be good. Like gold or emerald or purple repeating to itself, ‘No matter what anyone says or does, my task is to be emerald, my color undiminished.’” – Marcus Aurelius
Ni siku nyingine nzuri, siku mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Dhahabu itaendelea kuwa dhahabu hata kama watu watasema kwamba ni jiwe.
Mbwa hatobadilika kuwa paka kwa sababu watu ndiyo wanataka awe hivyo.
Mwembe utatoa maembe bila ya kujali watu wanataka utoe nini.
Kila kitu kwenye asili kinazalisha asili yake.
Ndivyo na wewe unavyopaswa kuendesha maisha yako, kwa kuishi asili yako bila ya kujali wengine wanasema au kufanya nini.
Mfano ni asili ya binadamu kuwa mwema, lakini wengi huruhusu kupoteza wema wao pale wengine wanapowasema au kuwafanyia vibaya.
Ukifanya hivyo unakuwa umewapa ushindi wao.
Ushindi kwako ni kuendelea kuwa kulingana na asili yako, bila ya kujali nini kinachoendelea.
Ijue asili yako na iishi asili hiyo kila wakati.
Kuwa na maisha ya aina moja wakati wote na siyo maisha ya kubadilika badilika kila mara kulingana na wanachosema au kufanya wengine.
Ijue misingi unayoisimamia na iishi kila wakati.
Uwe na siku bora sana ya leom siku ya kuishi asili yako, siku ya kuwa mwema bila ya kujali nini kinaendelea.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante kocha , jukumu langu ni kuwa mwema.
LikeLike