A man consists of body and soul. Thus often, especially in his youth, he is interested only in his body, but nevertheless, the most essential part of every man is not his body, but his soul. It is your soul that you must take care of, not your body. You must learn this over time, and remember that your real life is in your spirit, that is, in your soul. Save it from everyday dirt and do not let your flesh guide it; subdue your body to your soul, and then you will fulfill your destiny and live a happy life. —After MARCUS AURELIUS

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tunapaswa kuitumia siku hii vyema kwa kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

Wewe una vitu vitatu, mwili, akili na roho.
Roho ndiyo inakupa maana na sababu ya kuishi,
Akili inakuwezesha kufikiri na kufanya maamuzi,
Na mwili unatekeleza maamuzi hayo ili kifikia kusudi.
Vitu vyote hivi vitatu ni muhimu sana kwenye maisha yako.
Kikikosekana hata kimoja au kikawa dhaifu, maisha yako hayawezi kuwa sawa.

Lakini cha kushangaza umekuwa huvihudumii vitu hivi kwa usawa.
Unahangaika sana na mwili na kusahau akili na roho.
Unaulisha mwili wako kila siku, bila ya kukosa, lakini zipo siku hulishi akili na roho yako.
Unakazana kuuvalisha mwili wako nguo, huku akili na roho vikibaki uchi.
Na ndiyo maana vikwazo haviishi kwenye safari yako, kwa sababu unapuuza akili na roho.

Huoni aibu kusema huna muda wa kulisha akili yako (kwa kusoma na kujifunza),
Utasema bila wasiwasi huna muda wa kulisha roho yako (kwa kusali, kutahajudi, kushukuru),
Lakini kila siku unapata muda wa kulisha mwili wako (kwa vyakula na vinywaji), tena mara tatu kwa siku, na wakati mwingine unaulisha sumu kabisa.

Weka vipaumbele sahihi kwenye mwili, akili na roho.
Lisha vyote kila siku,
Fanya vyote kuwa imara,
Na wewe utakuwa imara kukabiliana na chochote kwenye maisha.

Uwe na siku bora leo, siku ya kuwa imara zaidi kwa kulisha mwili, akili na roho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania