“A person becomes happy to the same extent to which he or she gives happiness to other people.” —JEREMY BENTHAM

Ni siku nyingine mpya kwetu,
Tumepata nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Tuweke vipaumbele sahihi leo na kuvifanyia kazi.

Utakuwa na furaha kwa kiwango ambacho unawapa furaha wengine.
Hivyo furaha yako ni furaha ya wengine,
Ndivyo ilivyo kww kila kitu kwenye asili, unachopata wewe ni kile ambacho unawapa wengine.
Hivyo kama unataka kuwa na furaha, wawezeshe wengine kuwa na furaha pia.

Adui mkubwa wa furaha na hata mafanikio makubwa kwenye maisha ni ubinafsi,
Pale unapoweka maslahi yako mbele na kutojali wengine, ndiyo unajizuia kabisa usipate kile unachotaka.

Kuwa tayari kutoa kabla hujapokea na utapokea kwa viwango vikubwa mpaka utashangaa.
Ni kanuni ya asili kujaza palipo patupu, kurudishs kilichotolewa.
Itumie kanuni hii vizuri kwa kuanza kutoa chochote ambacho unataka kukipata.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwapa wengine furaha ili na wewe uwe na furaha pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania