“When you have doubts about what to do, just imagine that you might die at the end of that same day, and then all your doubts will disappear, and you will see clearly what your conscience tells you, and what is your true personal wish.” – Leo Tolstoy
Unapokuwa na mashaka,
Unapokuwa njia panda na hujui nini ufanye kati ya mengi unayotaka kufanya,
Ni rahisi sana kwako kupoteza muda, kwa sababu unajua kesho ipo.
Sasa hebu fikiria kwamba siku uliyonayo ndiyo siku ya mwisho kwako, mwisho wa siku hiyo unakutana na kifo chako.
Je bado utaendelea kuwa na mashaka?
Je bado utakaa njia panda ukijiuliza ufanye nini?
Hapana, hutapoteza muda wako,
Badala yake utafanya yale ambayo ni muhimu kwako na kwa wengine pia.
Anza kutumia nguvu hii ya kukiangalia kifo ili kikusaidie kufanya maamuzi sahihi na kuyafuata.
Kila unapojiambia hujui ufanye nini au kutaka kuahirisha kwamba utafanya kesho, jikumbushe kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kwako na jisukume kufanya kilicho sahihi.
Uwe na usiku mwema, usiku wa kuhakikisha unachagua na kufanya kilicho sahihi.
Kocha Dr. Makirita Amani.