“In order to change the nature of things, either within yourself or in others, one should change, not the events, but those thoughts which created those events.” – Leo Tolstoy
Kama unataka kubadili kitu chochote kwenye maisha yako, anza kwa kubadili fikra ulizonazo juu ya kitu hicho.
Kwa sababu fikra ndiyo zinazaa vitendo na vitendo ndiyo vinazaa tabia.
Ukianza kwa kubadili fikra zako, utaweza kubadili chochote kwenye maisha yako.
Usihangaike na kubadili matukio au matokeo, bali hangaika na kubadili fikra zako.
Huo ndiyo ufunguo muhimu kwenye kila kinachokuhusu.
Uwe na usiku mwema, usiku wa kujua ni fikra zipi zinakuwa kikwazo kwako na kuzibadili ili uweze kubadili maisha yako.
Kocha Dr Makirita Amani.