“First, tell yourself what you want to be, then act your part accordingly” – Epictetus
Kinachokukwamisha usifanikiwe ni kukosa msimamo,
Unajiambia unataka kuwa mtu fulani, lakini unachofanya ni tofauti na wanachopaswa kufanya watu wa aina hiyo.
Achana na tabia hiyo, fanya kama Epictetus alivyotushauri,
Kwanza jiambie unataka kuwa mtu wa aina gani, kisha kua.
Kama umejiambia unataka kuwa mfanyabiashara, fanya wanachofanya wafanyabiashara, ambapo ni kutafuta wateja, kuuza, kutoa thamani zaidi n.k
Umejiambia unataka kuwa mwandishi, kaa chini na andika, kwani unafikiri waandishi huwa wanafanya nini?
Mwalimu, fundisha,
Kiongozi, ongoza
Mkulima, lima
Mfugaji, fuga.
N.k
Usipoteze muda wako kuhangaika na yale yasiyohusika na kile unachotaka kuwa.
Na usijidanganye kwamba kujiambia utakuwa mtu fulani basi itatokea hata bila ya kuweka juhudi.
Jiambia unataka kuwa nani, kisha fanya kile ambacho watu wa aina hiyo wanafanya.
Uwe na usiku mwema, wa maandalizi ya kwenda kuwa yule uliyejiambia unataka kuwa.
Kocha Dr. Makirita Amani,