Rafiki yangu mpendwa,
Uandishi wa vitabu ni moja ya ndoto ambayo kila mmoja wetu anayo, ni moja ya alama ambazo ukiacha hapa duniani, hautasahaulika, kwani vizazi vijavyo vitajifunza mengi kutoka kwako.
Lakini ni wachache sana ambao wanapata nafasi ya kukamilisha ndoto hiyo ya kuandika kitabu hata kimoja tu.
Hii ni kwa sababu, unapokiangalia kitabu, hupati picha utaanzia wapi kukiandika mpaka umalize. Kwa mfano kitabu chenye urefu wa kawaida ni kurasa 250 mpaka 300 ambapo kwa maneno ni wastani wa maneno elfu 60.
Sasa kuandika maneno elfu moja tu ni shughuli kwa wengi, vipi maneno elfu 60? Hapo ndipo wengi wanaona ni kazi kubwa na hivyo kuahirisha wakiamini kuna siku watakuja kupata nguvu ya kuandika kitabu wanachopanga kuandika.
Vipi kama leo nitakuambia kwamba unaweza kuandika kitabu chenye maneno zaidi ya elfu 60 ndani ya siku 30 pekee?
Sasa sitaki nikueleze mimi, bali nataka aliyefanya hivyo akueleze kupitia ushuhuda wake unaokwenda kusoma hapo chini.
Siku 30 za GAME CHANGERS kwangu zimekuwa ni za tofauti sana katika maisha yangu.
- Kuandika kitabu chenye maneno zaidi ya 81,000+ sio jambo dogo kwa kuwa katika maisha yangu sijawahi kuwaza wala kuandika kitabu.
- Kuweza kuwakutanisha kwa mara moja watumishi zaidi ya 80 wa benki za NMB, CRDB, TPB na NBC na kunisikiliza. Kwangu hilo ni jambo kubwa sana kwakuwa sijawahi kufanya hivyo katika kipindi chote cha utumishi wangu.
Nimejifunza mengi sana toka kwa wenzangu na kocha pia.
Nimejifunza kuweka mipango na kuitekeleza kila siku.
Matarajio yangu ni kupiga hatua kubwa sana mwaka huu katika uandishi na kufundisha makundi mbalimbali.
Kweli kabisa Game Changer Program, haikuwachi kama ulivyokuwa. Najiona kabisa kwa kiasi cha tshs 300,000 ni kidogo sana ukilinganisha na maendeleo endelevu niliyoyapata na nitakayozidi kupata. Asante sana kocha, asante sana Palmo, Symphrosa na Sebastian.
Daniel Zake
Daniel Zake ni mmoja wa watu wanne walioshiriki programu ya GAME CHANGERS kwa msimu wa mwezi Januari 2020. Katika programu hii, Zake alikuwa na majukumu makuu mawili, kuandika kitabu na kutoa mafunzo ya kujitambua kwa vijana wa makundi mbalimbali.
Kwa mpango bora kabisa ambayo tuliuweka pamoja, pamoja na mwongozo wa Kocha na msukumo wa washiriki wengine kwenye programu hii, Zake aliweza kutekeleza vizuri mipango hiyo.
Hajawahi kuandika kabisa kwenye maisha yake, lakini ndani ya siku 30 ameweza kuandika maneno zaidi ya elfu 80 ambacho ni kitabu kilichoshiba hasa.
SWALI MUHIMU KWAKO.
Rafiki, umeusoma ushuhuda wa mwenzetu hapo juu, ambao unatia moyo na kuhamasisha. Hapa nina swali muhimu sana kwako, je na wewe unataka kutengeneza matokeo makubwa kama hayo kwenye maisha yako?
Je kuna kitu kikubwa umekuwa unapanga kufanya lakini hukianzi? Mfano kuanza biashara, kuandika kitabu, kukuza biashara au kingine chochote kwenye maisha yako?
Kama jibu ni ndiyo, kwamba unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, basi nina habari njema sana kwako. Msimu wa GAME CHANGERS PROGRAM MACHI 2020 umefunguliwa na kuna nafasi chache ambazo zimebaki.
Karibu sana ushiriki programu hii kwa mwezi Machi na upate nafasi ya kufanya makubwa sana kwenye maisha yako, ambayo hujawahi kuyafanya kabisa kwenye maisha yako.
UTARATIBU WA GAME CHANGERS.
GAME CHANGERS ni programu maalumu ya ukocha ambayo inaendeshwa na Kocha Dr Makirita Amani ambayo inawalenga wale wanaotaka kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao na kwa muda mrefu.
Programu hii inakupa manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo ni COACHING (ambapo unapata mwongozo wa kocha) na MASTER MIND (ambapo unapata msukumo wa wengine wanaofanya makubwa kama wewe). Hizi ni nguvu mbili ambazo zinakuwezesha kufanya makubwa sana zikitumika pamoja.
Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne ili kutoka pale ulipokwama sasa na kupiga hatua kubwa.
Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.
Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao. Ndani ya kundi hili kila siku kunakuwa na mijadala ya hatua ambazo kila mtu anapiga kwenye mipango aliyojiwekea kwa wiki husika.
Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.
Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.
Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.
Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.
NAFASI ZA KUSHIRIKI GAME CHANGERS MACHI 2020.
Rafiki, kama nilivyokushirikisha kwenye utangulizi, programu hii ya GAME CHANGERS huwa inaendeshwa kwa misimu, na msimu mmoja unachukua siku 30 ambazo ni mwezi mmoja.
Tunakwenda kuanza msimu mwingine wa programu hii ya GAME CHANGERS mwezi Machi 2020, kuna nafasi tano pekee za kushiriki programu hii kwa msimu huo wa mwezi Machi. Hivyo karibu sana uchukue hatua sasa.
HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUSHIRIKI GAME CHANGERS.
Kama kwa kusoma hapa umeona GAME CHANGERS ni kitu unachohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa (na ni kitu unachohitaji kweli), basi chukua hatua sasa ili kuweka nafasi yako ya kushiriki programu hii.
Hatua ya kuchukua ni kutuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako na maelezo kwamba utashiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020.
Kwa kufanya hivi unajihakikishia nafasi ya kushiriki programu hii na kunufaika nayo.
Chukua hatua sasa kwa sababu nafasi zilizopo ni chache (tano pekee) na uhitaji ni mkubwa. Tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.
ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA MSIMU WA MACHI 2020.
Ada ya kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.
Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.
Msimu wa mwezi Machi wa programu hii ya GAME CHANGERS 2020 utaanza rasmi siku ya jumamosi tarehe 07/03/2020 na kumalizika siku ya jumamosi ya tarehe 04/04/2020.
Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/= kabla ya tarehe 03/03/2020. Pia tuma mapema taarifa ya ushiriki ili uweze kupata nafasi hii, kwa kutuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba utashiriki GAME CHANGERS JANUARI 2020.
Nafasi za kushiriki programu hii kwa mwezi machi ni 5 pekee, na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.
Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache chache sana.
Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020 ni tarehe 03/03/2020. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 05/03/2020 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.
Tarehe 07/03/2020 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.
Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.
Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.
Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.
Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,