Kazi yoyote unayoifanya, ithamini sana.
Anza wewe mwenyewe kuipenda, kuikubali na kuifanya kwa moyo wako wote.
Jitume katika kuifanya, ifanye kwa ubunifu na utofauti mkubwa, asiwepo yeyote ambaye anaweza kuifanya kuliko wewe.
Halafu watake wengine nao waithamini kazi yako, usikubaliane na wale wanaoidharau kazi yako, wanaoona hakuna unachofanya.
Iwe ni mwajiri au mteja, kazana kumpa thamani na tegemea na yeye akupe thamani pia. Kama hathamini huna haja ya kuendelea kumpa kazi yako, tafuta yule anayethamini na mpe.
Kazi ndiyo kitu pekee ambacho kina historia ya kuwatoa watu kwenye umasikini na kuwafikisha kwenye utajiri mkubwa, na siyo kazi fulani pekee, bali kazi yoyote ile ikifanyika vizuri, ina nguvu ya kuleta matokeo makubwa kwa mfanyaji.
Ile kazi ambayo hakuna mwingine ambaye yuko tayari kuifanya, ndiyo kazi yenye thamani kubwa kwako kama utaifanya vizuri, maana hapo kuna fursa kubwa ya kutoa matokeo ya tofauti.
Usifanye kazi yako kwa sababu tu unataka kulipwa, au kwa sababu huna kingine cha kufanya, bali ifanye kwa upekee, ifanye kama ndiyo kitu pekee unachopaswa kufanya, na kwa hakika ndiyo kitu pekee unachopaswa kufanya wakati unafanya.
Kila kinachohusu kazi yako ni muhimu, ni nafasi ya wewe kufanya kwa ubora zaidi, ni nafasi ya wewe kutia mchango wako kwa wengine.
Ni kazi yako. Ni wajibu wako. Ifanye.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kazi inakupa heshimu kwenye jamii
Sio wote wanauwezo wa kufanya kazi hasa wanawake
Asante sana kocha kutukumbusha
Kufanya kazi kwa ubora wa hali juu .
LikeLike