Biashara inafanikiwa kwa vitu vinavyotoka na siyo vinavyoingia.
Kwa maneno mengine biashara inafanikiwa kwa fedha inayoingia na siyo inayotoka.
Au kama bado hujaelewa vizuri, biashara inafanikiwa kwa kile inachouza na siyo inachonunua.
Huu ni msingi muhimu sana wa kuelewa na kukumbuka, kwa sababu wengi wamekuwa wanausahau na ndiyo chanzo cha biashara nyingi kuingia kwenye changamoto.
Uzito hauwekwi eneo sahihi.
Ni rahisi sana kununua kuliko kuuza, na watu wanapenda kufanya vilivyo rahisi, hivyo watanunua zaidi.
Na siyo tu kununua bidhaa au huduma zinazouzwa, bali kununua vitu ambavyo ni vya matumizi kwenye biashara, ambavyo haviuzwi.
Ni rahisi sana kutoa fedha, lakini kuingiza kunahitaji kazi, hivyo watu wakishawishiwa au kujishawishi kidogo kwamba wanahitaji kitu fulani, basi wanatoa fedha kukinunua.
Weka uzito kwenye eneo sahihi, weka kipaumbele kwenye kutoa vitu, kwenye kuuza, kwenye kuingiza fedha na siyo kinyume chake. Kila siku kazana kutoa zaidi, kazana kuuza zaidi na utaweza kuikuza biashara yako zaidi.
Kabla hujafanya maamuzi yoyote kwenye biashara jiulize unatoa fedha au unapokea fedha? Kama unapokea fedha endelea mara moja, kama unatoa fedha jisubirishe kwanza.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kweli jitafakari kabla ujaamua kufanya Chochote kwenye biashara
Asante sana kocha
LikeLike