Habari za leo rafiki yangu mpendwa,
Karibu kila mtu anajua ni nini hasa anachotaka kwenye maisha yake, lakini ni wachache sana wanaopata kile wanachotaka. Wengi wanaendesha maisha yao kwa kupokea kile kinachopatikana na siyo kupata wanachotaka.
Siku moja mtu aliniandikia email akiniambia wewe unashauri watu wawe na biashara wakati hali ya uchumi ni ngumu na biashara nyingi zinafungwa, huoni unawapoteza? Nikamjibu kumwambia hali ya uchumi siyo inayofanya biashara zife na kufungwa, bali namna watu wanavyokuwa wanafanya biashara zao.
Nikampa mfano kwamba katika watu ambao ninawakochi kwenye biashara zao, wote biashara zao zinakwenda vizuri sana. Hakuna mtu ninayemkochi ambaye analalamika kwamba biashara yake itakufa. Na kinachowafanya watu hawa wawe tofauti ni kwa sababu wanaziendesha biashara zao kwa mfumo sahihi, mfumo ambao haijalishi nini kinaendelea, biashara hizo zinaendelea kusimama na kuwa imara.
Ninachoendelea kujifunza ni kwamba watu wengi hawajajitoa kweli kupata kile wanachotaka, hivyo inakuwa rahisi sana kwao kubeba sababu zinazotolewa na watu wengine na kuzifanya kuwa sababu zao. Kwa kuwa kila mtu anasema hali ni ngumu, basi na wao wanabeba hiyo sababu. Mfano kwa miaka 10 mtu amekuwa anajiambia ataanzisha biashara lakini haanzishi, ila miaka hii ya karibu sababu yake kubwa ni hali ngumu. Je vipi kwa miaka mingi iliyopita ambapo sababu haikuwa hali ngumu? Bila shaka mtu huyo alikuwa na sababu nyingi zinazoonekana za maana kweli, lakini hazijawa na manufaa kwake.
Nimechoka kuwaona watu wengi wakikubali maisha ya kawaida wakati ndani yao wana uwezo wa kuwa na maisha ya juu, maisha wanayoyataka. Nimechoka kuwaona watu wakilalamika kwa mambo ambayo kila mtu anayalalamikia wakati hawakuwa wanachukua hatua hata kabla ya watu kuja na malalamiko hayo.
Na uchovu huu umenipeleka kukuandalia makala hii ambayo itakwenda kukata mzizi wa fitina, itakwenda kukupa mwanga wa uhakika wa hatua zipi uchukue na uache kusingizia sababu za wengine. Ukishasoma makala hii, unachopaswa kufanya ni kuchukua hatua tu, weka sababu pembeni na uchukue hatua.
Kuna nguvu kubwa tatu za kukuwezesha kupata chochote unachotaka. Nguvu hizo ni kubwa na zinashinda kila aina ya sababu ambayo umekuwa unajipa. Kwa kujua na kuzitumia nguvu hizo tatu, utaweza kuyabadili maisha yako kiasi ambacho kitawastua sana wengi na kuona labda kuna nguvu zisizo za kawaida unatumia.
Leo nakwenda kukujulisha nguvu hizo tatu, na kazi yako ni kuziweka kwenye matendo ili uweze kunufaika nazo.
Lakini kabla hujajua nguvu hizi tatu, lazima kwanza ujue nini unataka. Nguvu hizi hazitakusaidia wewe kujua nini unachotaka. Hivyo lazima ujue nini hasa unachotaka kwenye maisha yako, lazima ujue nini kinakunyima usingizi usiku, nini ambacho hakitoki kwenye fikra zako. Ukishajua kitu hicho, basi unaweza kuzitumia nguvu hizi tatu na kwa hakika utapata kitu hicho.
Zifuatazo ni nguvu tatu za kukuwezesha kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Nguvu ya kwanza; SHAUKU.
Shauku ndiyo nguvu ya kwanza ya kukuwezesha kupata kile ambacho unataka kwenye maisha yako. Shauku ni ule msukumo wa ndani wa kukutaka upate kile unachotaka. Msukumo ambao hauondoki wala kupungua. Shauku ina nguvu kubwa ya kukusukuma kufanya mambo ambayo wengine wanaogopa, lakini kwako yanaonekana kawaida.
Watu wengi wamekuwa wanategemea hamasa iwafikishe kwenye mafanikio makubwa, lakini tatizo la hamasa ni huwa haidumu, mara kwa mara inabidi uchochee upya hamasa yako. Lakini shauku huwa haipungui wala kuhitaji kuchochewa, shauku unakuwa nayo muda wote na hii ndiyo inakusukuma wewe kupiga hatua zaidi.
Shauku inatokana na ile sababu kubwa inayokusukuma kupata unachotaka, ile KWA NINI inayokufanya wewe upambane kupata unachotaka. Kwa nini zinatofautiana kwa watu, wapo ambao wanafanya kwa sababu wamejitoa kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi, wapo ambao wanafanya ili kuwaonesha wengine wanaweza na kadhalika.
Hakikisha una msukumo mkubwa ndani yako wa kukupeleka kwenye kile unachotaka, kwa sababu bila ya msukumo huu, hakuna nguvu nyingine itakayoweza kukusaidia kupata unachotaka.
Nguvu ya pili; MWONGOZO.
Ili kupata unachotaka, unahitaji kupata mwongozo kutoka kwa mtu mwingine. Mtu huyo anaweza kuwa kocha, menta au mshauri ambaye anakusimamia ufike kule unakotaka kufika.
Iko hivi rafiki, sisi binadamu ni wavivu na hatupendi kujitesa. Tunaweza kuweka mipango mikubwa na mizuri sana, lakini tunapokutana na ugumu ni rahisi kuacha na kujiambia haiwezekani au hatuwezi.
Lakini unapokuwa na mtu wa pembeni ambaye anakuangalia na kukusimamia, kwanza hutataka kumwangusha, hivyo utajisukuma zaidi na pili yeye mwenyewe hatakubaliana na wewe kirahisi, hivyo itakubidi ujaribu tena na tena na tena kabla hujasema haiwezekani.
Watu wengi wamekuwa wanajiwekea malengo peke yao, na asilimia 99 wamekuwa hawayafikii. Ila wale wanaoweka malengo na kuwa na mtu wa kuwasimamia kwenye malengo yao, zaidi ya asilimia 90 wanayafikia.
Hii ndiyo nguvu kubwa iliyopo kwa kuwa na mwongozo. Kwa sababu pia mtu anayekuongoza anaweza kukushauri vizuri pale ambapo unakuwa umekwama. Ni rahisi kuona makosa ya mchezaji aliyepo uwanjani ukiwa nje ya uwanja, lakini yule aliyepo uwanjani anaweza asione kwa urahisi. Kuna makosa unaweza kuwa unafanya kwenye maisha yako lakini huyaoni, ila unapokuwa na mtu anayekusimamia, atakuonesha makosa hayo kwa urahisi na utaweza kupiga hatua sana.
Unahitaji kuwa na mtu wa kukusimamia kwenye malengo na mipango uliyonayo ambaye atakusukuma kuyafikia.
Nguvu ya tatu; JUMUIA.
Nguvu ya tatu ya kukuwezesha kupata chochote unachotaka ni jumuia, yaani watu wanaokuzunguka.
Rafiki, watu wanaokuzunguka wana nguvu kubwa sana kwako, hata kama hujui. Watu hao, hasa wale wa karibu, wana ushawishi mkubwa kwako. Kama wanaokuzunguka wana mtazamo hasi wa kuona mambo hayawezekani, na wewe pia utajikuta umebeba mtazamo huo, hata kama utakuwa unapingana nao kiasi gani.
Na kama watu wanaokuzunguka wana mtazamo chanya wa inawezekana, na wewe pia utabeba mtazamo huo. Nguvu hii ya wanaokuzunguka ni nguvu kubwa sana unayopaswa kuwa nayo makini. Wengi wamekuwa wanapuuza nguvu hii, wakiamini wanaweza kuzungukwa na watu wa aina yoyote lakini wakafanikiwa. Hicho kitu hakipo kabisa, kama haujazungukwa na watu sahihi, huwezi kufanikiwa. Ni asili ya binadamu, hatuwezi kwenda juu zaidi ya wale ambao wanatuzunguka.
Hivyo ili kupata kile unachotaka kwenye maisha, tafuta watu wanapiga hatua kwenye maisha yao na uwe nao karibu. Watu ambao wanaamini kwenye ndoto kubwa na wasiokata tamaa. Watu hawa watakupa nguvu ya kuendelea hata pale unapokutana na magumu na changamoto.
Rafiki, tumia nguvu hizi tatu; SHAUKU, MWONGOZO na JUMUIA kukuwezesha kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, na hakuna chochote kinachoweza kukuzuia.
NJIA BORA YA KUZIPATA NGUVU HIZI TATU.
Rafiki, najua unaweza kuwa njia panda, ukijiuliza unawezaje kuzipata na kuzitumia nguvu hizi tatu, huenda hujui unawezaje kuibua shauku kubwa ndani yako, huenda hujui utapataje mtu mzuri wa kukuongoza na huenda huoni watu wazuri wa kukuzunguka kwenye safari yako ya kupata unachotaka. Kwa kuona ugumu wa kupata vitu hivi vitatu, huenda unaona itakuwa vigumu kwako kufanikiwa.
Hapo ndipo mimi kocha wako ninapoingia kwenye maisha yako. Mimi kama kocha wako nina uwezo wa kukupa nguvu hizo tatu na ukaweza kuzifanyia kazi ili kupata chochote unachotaka.
Na kwa programu tunayokwenda kuianza karibuni ya GAME CHANGERS, unakwenda kuzipata nguvu hizi tatu kwa wakati mmoja na kwa siku 30, kitu ambacho kitawasha moto mkubwa sana ndani yako.
Kwenye programu hii, kwanza utapata nafasi ya kujibu maswali yanayoibua ile shauku kubwa iliyopo ndani yako, na baadaye unapata nafasi ya kuwa na maongezi kwa simu na kocha, ambayo yanalenga kuibua shauku kubwa iliyopo ndani yako, ambayo itakuwa ndiyo moto wako mkuu wa mafanikio.
Pili utapata mwongozo wa karibu wa kocha, ambaye atakuwa anakupa misingi sahihi ya kufuata, atakuwa anakuonesha makosa unayofanya na kukusaidia kutatua changamoto unayokutana nazo katika safari yako. Kocha atakusukuma zaidi ili usiishie njiani.
Tatu utazungukwa na watu wengine ambao wanataka kupiga hatua kama wewe. Na tafiti zimekuwa zinaonesha wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka. Kwenye programu hii utazungukwa na watu watano wanaotaka kupiga hatua kama wewe. Watu hawa watakupa hamasa ya kupiga hatua zaidi na pia utajifunza kutoka kwao na kuweza kupiga hatua zaidi.
Rafiki, nguvu hizo tatu utazipata kwenye programu ya GAME CHANGERS, programu ambayo inakujia mwezi MACHI 2020.
NAFASI MOJA YA KIPEKEE YA KUSHIRIKI PROGRAMU YA GAME CHANGERS MACHI 2020.
Rafiki, siku chache zilizopita, nilikupa taarifa kwamba nafasi za kushiriki programu ya GAME CHANGERS kwa msimu wa MACHI 2020 zimeshajaa.
Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha ya kwamba kuna nafasi moja imepatikana. Mtu aliyekuwa amedhibitisha kushiriki programu hii ameshindwa kuendelea. Hivyo nafasi yake iko wazi kwa ambaye anaihitaji.
Najua wengi mlipenda kupata nafasi hizi, ambazo zipo tano pekee lakini mkawa mmezikosa. Sasa imepatikana nafasi moja kwa ambaye yupo tayari basi tuwasiliane mara moja kwa wasap namba 0717396253 ili upate maelekezo ya kushiriki kwenye programu hii.
Ada ya kushiriki kwenye programu hii ni tsh 300,000/= (laki tatu) na kwa siku 30 za mwezi juni tutafanya kazi pamoja ambayo itakuwezesha kujijengea msingi wa kupata chochote unachotaka.
Kila siku utajifunza misingi ya mafanikio makubwa, na kila juma tutakuwa na simu ya pamoja ambapo utaeleza hatua unazopiga pamoja na kushauriwa vizuri na wengine pamoja na kocha.
Hii ni programu ambayo inakwenda kuacha alama kubwa sana kwenye maisha yako, kwa sababu najua nguvu ya nguvu hizi tatu.
Nimepata bahati ya kufanya kazi na watu wengi kupitia kuwakochi, na nimeona jinsi ambavyo watu wanabadilika sana kwa kipindi kifupi. Wapo watu ambao walikuwa na biashara ambazo waliamini ni ngumu na haziwezi kukua, lakini baada ya muda biashara zinakua zaidi. Wapo ambao waliamini hawawezi kuandika kitabu, lakini wameweza kukamilisha uandishi wa vitabu vyao. Wapo ambao wamekuwa wanaweka malengo kila mwaka lakini hawayafikii, lakini kwa kufanya nao kazi ya kuwakochi wanafikia malengo yao kwa muda mfupi kuliko walivypopanga.
Rafiki, kama kuna hatua kubwa unataka kupiga kwenye maisha yako lakini unakwama au hupati nguvu ya kuanza, basi programu hii ya GAME CHANGERS kwa msimu wa MACHI 2020 ni kwa ajili yako, usikubali kabisa ikupite.
Tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap namba 0717396253 na utapewa maelekezo ya kujiunga na programu hii na mwezi machi utakuwa mwezi wa uhuru mkubwa kwenye maisha yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020 uweze kuzitumia nguvu hizi tatu kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr. Makirita Amani,