“You have no responsibility to live up to what other people think you ought to accomplish.
I have no responsibility to be like they expect me to be. It’s their mistake, not my failing.” – Richard Feynman
Kila mtu anajua mtu mwingine anapaswa kuwaje, anapaswa kufanya nini na maisha yake ayaendesheje.
Lakini ni wachache sana ambao wanajua hayo kuhusu maisha yao wenyewe.
Sasa wewe kuwa kati ya hao wachache, kwa kujua unataka nini, unapaswa kufanya nini na maisha yako uyaendesheje.
Kisha puuza kabisa yale ambayo wengine wanakupangia.
Siyo wajibu wako kuishi kama vile ambavyo wengine wanataka uishi,
Siyo wajibu wako kuwa kama wengine wanavyotaka uwe,
Ni maisha yako, siyo yao, fanyia kazi vipaumbele vyako, siyo wao.
Na ukishindwa kuwa kama wao wanavyotaka, siyo tatizo lako, bali ni kushindwa kwao wenyewe.
Kwa kujua na kulielewa hili, unapata uhuru mkubwa wa kuendesha maisha yako vile unavyotaka na kupambana na yale ambayo ni muhimu kwako.
Hufanyi chochote ili kuwafurahisha wengine, bali unafanya kwa sababu ni muhimu na inakupeleka kula unataka kufika.
Nenda kayaishi maisha yako leo, na puuza yale ambayo wengine wanataka uwe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania