“People are rational creatures. Why do they seem capable of using violence so much more easily than reason in their interactions with each other?” – Leo Tolstoy

Sisi binadamu ni viumbe wa kufikiri,
Una uwezo mkubwa wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi kulingana na hali ambayo unaipitia.
Lakini mara nyingi umekuwa unaacha kutumia uwezo huo na badala yake unakazana kutumia nguvu pekee.

Unapokabiliana na wengine, silaha yako kuu ni fikra zako,
Ukiweza kuzitumia vizuri, unaweza kushawishi chochote kile kwa yeyote yule.
Lakini cha kushangaza wengi wanakimbilia kitumia nguvu na fujo wanapokabiliana na wengine.
Wewe usiingie kwenye kundi hili la wanaoacha silaha kuu na kuhangaika na vitu vingine.
Badala yake itambue silaha yako kuu na itumie vizuri kwenye kila unachokabiliana nacho.

Hata unapojikuta kwenye matatizo na changamoto, anza ma fikra zako kwanza kabla hujaangalia kingine chochote.
Ukianza kwa kuweka fikra zako sawa, mengine yote yanakaa sawa.
Lakini ukianza kuhangaika na mengine na kuachana ma fikra, unazidi kuongeza matatizo na changamoto.

Kufikiri ndiyo kinachokutofautisha wewe na viumbe wengine, ndiyo silaha yako kuu, ijue na kuitumia. Nenda kafikiri vyema leo ili uweze kukabiliana na chochote kinachokuja mbele yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania