“If beautiful art does not express moral ideas, ideas which unite people, then it is not art, but only entertainment. People need to be entertained in order to distance themselves from disappointment in their lives.” —IMMANUEL KANT

Sanaa ni kitu kinachowaleta watu pamoja,
Ni kitu chenye maadili na misingi yake, ambayo inawawezesha watu kufikiri kwa kina na kuchukua hatua sahihi.
Burudani ni kitu kinachowafanya watu wasahau shida zao kwa muda.
Ni kitu kinachowafubaza watu na kuwazuia wasifikiri, hivyo wasione matatizo waliyonayo.

Watu wengi wamekuwa wanachanganya sanaa na burudani, wakifikiri ni kitu kimoja.
Watu wengi wamekuwa wanahangaika na burudani, wakidhani ni sanaa.
Ushairi ni sanaa pale unapokuwa umebeba ujumbe wenye msingi fulani. Lakini pale unapokuwa ni wa kufurahisha tu, unageuka kuwa burudani.
Mchoro ni sanaa pale unapokuwa na ujumbe fulani ambao mtu anaweza kuung’amua na kuutumia vyema, lakini unapokuwa ni mchoro wa kusisimua tu, unaishia kuwa burudani.

Kwa kujua haya, kazana na sanaa na achana na burudani.
Unahitaji kuipa akili yako kazi, ili iwe imara zaidi na iweze kufanya maamuzi sahihi.
Usikubali kila mara kukimbilia kwenye burudani, kwa sababu kusahau shida zako kwa muda hakuzipunguzi, bali kunazipa nafasi ya kukua zaidi.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kujishughulisha na sanaa zaidi na siyo burudani pekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania