“A person who overeats cannot fight laziness; and a lazy man cannot fight sexual dissipation. All spiritual teachings start with restrictions, with control of the appetite.” – Leo Tolstoy

Moja ya tamaa ambazo zinawaangamiza wengi bila ya wao kujua ni tamaa ya chakula.
Watu wamekuwa wanakula kupitiliza, kitu ambacho kinapeta madhara makubwa kwenye miili yao.

Kama unataka kuwa na udhibiti bora wa maisha yako, anza kudhibiti ulaji wako.
Kula pale tu unapokuwa na njaa,
Na usile mpaka ukashiba kabisa, maliza kula ukiwa bado una hamu ya kuendelea kula.
Yaani kula kwa kiasi, kabla hujashiba kabisa, acha, usiendelee tena kula.

Ukiweza kujidhibiti kwenye ulaji (hasa wa vitu vitamu) utaweza kujidhibiti kwenye tamaa nyingine kama za ngono na hivyo utaweza kuwa na maisha tulivu.
Jifunze kukataa chakula hata kama una njaa, kwa kuchagua tu kukataa na siyo kwa sababu nyingine yeyote.
Kwa kufanya hivyo unajijengea nidhamu bora sana na hutasumbuliwa na tamaa.

Jaribu hili mara moja moja, ukiwa umeenda kwenye sherehe au shughuli yoyote ambapo kuna vyakula vizuri vimeandaliwa, nenda ukiwa na njaa kabisa, kisha unapofika wakati wa chakula, usichukue chakula, wewe kunywa maji tu. Watu wakikuuliza kwa nini wajibu umekamatwa na tumbo la ghafla.
Lakini kaa katikati ya watu hao, woane wakiwa wanakula kuku na vitu vingine vitabu, ipate harufu na ikutoe mate, jua kabisa unaweza kwenda kuchukua chakula lakini umechagua kutokula leo.
Ukiweza kufaulu zoezi hilo, utakuwa na nidhamu binafsi nzuri na kuweza kujidhibiti.

Unafikiri kwa nini kila imani ina utaratibu wa watu kufunga kula?
Hakuna kitu kinachoweza kukupeleka kwenye dhambi au makosa kama ulaji wa kupitiliza.
Dhibiti tamaa yako kwenye ulaji na utaweza kudhibiti mengi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania