“He who always listens to what other people say about him will never find inner peace.” – Leo Tolstoy

Kama mara zote unasikiliza kile ambacho watu wanasema kuhusu wewe, hutaweza kuyaishi maisha yako.
Utaishia kuishi maisha ya wengine na hilo halitakupa utulivu unaohitaji kwenye maisha.

Hakuna mtu mwingine anayeyajua maisha yako zaidi yako,
Hakuna anayejua nini hasa unachotaka,
Hakuna ajuaye uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Vyote hivi ni siri yako, ni hazina yako ambayo ukiweza kuitumia vizuri, utafanya makubwa sana.

Hebu fikiria kama watu matajiri wangekuwa wanasikiliza kila ambacho masikini wanasema kuhusu wao, wangeshaachana na utajiri wao na kujiunga na umasikini wa wengine.
Lakini hawaondoki kwenye utajiri wao kwa sababu wanajua nini wanataka na hawasikilizi chochote tofauti na wanachotaka.

Hivi hujawahi kushangaa jinsi ambavyo kila mtu anajua wengine wanapaswa kuendesha vipi maisha yao, lakini wao wenyewe hawawezi kuendesha maisha yao?
Je hii ndiyo aina ya watu unaotaka kuwasikiliza na kufuata wanachosema?

Jua kwa hakika nini unataka kwenye maisha yako,
Jua nini unapaswa kufanya ili kupata unachotaka,
Kisha FANYA.
Usihangaike na wale wanaokukwamisha au kukukatisha tamaa kwenye kile unachotaka. Wewe pambana.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania