“If you accept the obstacle and work with what you’re given, an alternative will present itself—another piece of what you’re trying to assemble.” – Marcus Aurelius
Usisubiri mpaka upate kila unachotaka ndiyo uanze kufanya ulichopanga kufanya,
Badala yake tumia kile kilichopo, kile ulichonacho sasa na anza.
Uzuri ni kwamba, ukishaanza kufanya, fursa nyingi zaidi zitajitokeza mbele yako na utaona njia mbadala za kufanya na kupata kile unachotaka.
Kusubiri mpaka kila kitu kiwe sawa, ni kujichelewesha.
Anzia hapo ulipo, anza na ulichonacho.
Ni kanuni ya asili kwamba kitu kilichotulia kitaendelea kutulia na kilichopo kwenye mwendo kitaendelea na mwendo mpaka pale nguvu ya nje itakapotumika kubadili hali ya kitu.
Vunja hali ya kutulia na anzisha mwendo na hakikisha mwendo huo unaendelea, haukwami popote.
Mwendo utazalisha mwendo, ambao utakuonesha fursa zaidi.
Uwe na siku bora, siku ya kuanza na kile ulichonacho na siyo kusubiri.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania