“Do not wish for death just because your life is hard. All the burdens on your shoulders will help you fulfill your destiny. The only way to get rid of your burdens is to live your life in such a way that you fulfill your destiny.” —RALPH WALDO EMERSON

Kifo siyo suluhisho la maisha magumu.
Usitamani kufa kwa sababu maisha magumu, usijiambie ni heri kufa kuliko kuendelea na ugumu wa maisha ulionao.
Kwa sababu ugumu wa maisha unaopitia sasa, mzigo mzito ulioubeba ndiyo unaokufikisha kwenye kusudi la maisha yako.
Magumu unayopitia ndiyo yanayapa maisha yako maana.

Njia pekee ya kuondokana na ugumu wa maisha, njia pekee ya kupunguza mzigo na kuyafanya maisha yako kuwa rahisi,
Ni kuyaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Kujua kusudi la maisha yako na kuishi maana yake.

Ukijua kwa nini uko hapa duniani na ukajua mchango bora unaotoa kwa wengine, ugumu wa maisha hautakuwa kitu cha kukufikirisha wewe.
Utauona ugumu wa maisha zaidi ukiwa mbinafsi, ukijiangalia wewe mwenyewe zaidi ya unavyowaangalia wenyewe, utaona kila kitu kinakuumiza wewe.
Lakini ukianza kujali wengine, ukiangalia jinsi unavyohusika kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora, unasahau magumu yako na unakuwa na cha kukusukuma kuendelea zaidi.

Hivyo kama kila siku unayaona maisha yako yanazidi kuwa magumu, basi jua umezidi ubinafsi, unajiangalia wewe mwenyewe zaidi kuliko unavyowaangalia wengine.
Jua kusudi la maisha yako na liendee, jua maana ya maisha yako na iishi na hakuna ugumu utakaokusumbua.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania