“There is no need for temples, no need for complicated philosophies. My brain and my heart are my temples; my philosophy is kindness.” – Dalai Lama
Ili maisha yako ya kiimani yakamilike, unahitaji vitu viwili, hekalu na falsafa.
Hekalu ni pale roho yako inapoishi,
Falsafa ni kile roho yako inaamini na kusimamia.
Sasa watu wameenda mbali katika kutafuta mahekalu na falsafa ngumu mno.
Hivi ndivyo dini nyingi zilivyozaliwa,
Mwishowe zinawafanya watu kuwa watumwa badala ya kuwaweka huru.
Huhitaji kwenda mbali kutafuta mahekalu,
Bali una mahekalu ambayo tayari unayo.
Mwili wako na akili yako ni mahekalu muhimu kwako,
Vitunze hivi, viweke safi na imara wakati wote,
Kwa kuwa ndiyo vinabeba roho yako.
Huwezi kuwa huru au tulivu kama mwili au akili havipo sawa.
Pia huhitaji kuhangaika na falsafa ngumu na usizozielewa,
Wema na upendo ni falsafa tosha kwako,
Kila mtu anauelewa wema na upendo,
Na vinaweza kumnufaisha kila mtu,
Huku vikikupa wewe utulivu mkubwa.
Ukisimamia wema na upendo kwenye maisha yako, hakuna kitakachokusumbua.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuboresha mahekalu yako (mwili na akili) na kuimarisha falsafa yako (wema na upendo).
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania