“Help should be mutual. Moreover, those who accept help and assistance from their brothers should pay them back, not only with money, but with love, respect, and gratitude.” – Leo Tolstoy

Sisi jamii ya binadamu, tumefanikiwa kuliko viumbe wengine wote hapa duniani kwa sababu ya ushirikiano wetu.
Kila mtu kuna kitu anaweza kutoa kwa wengine, na ambacho anaweza kupokea.
Ushirikiano mzuri na mahusiano yanayodumu ni yale ambayo kila mtu ana kitu cha kutoa na kupokea.

Ukiwa mtu wa kupokea tu unageuka kuwa mzigo kwa wengine na wanachoka kukupa.
Ukiwa mtu wa kutoa tu unawageuza wengine kuwa watumwa kwako na watajisikia vibaya.
Linganisha vizuri kutoa na kupokea ili uweze kuwa na mahusiano mazuri pamoja na ushirikiano bora.

Una vingi vya kutoa kwa wengine, siyo tu fedha, bali kazi yako, vipaji vyako, ujuzi wako, uzoefu wako, heshima, upendo, shukrani na mengine mengi.
Pianuna vingi vya kupokea kwa wengine, siyo tu fedha zao bali kazi zao, vipaji vyao, ujuzi wao, uzoefu wao, heshima, upendo, shukrani na mengine mengi.

Kuwa tayari kutoa na kuwa tayari kupokea, hivyo ndivyo unakuwa binadamu bora, unayejali na kujaliwa na wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania