Kuna sababu kwa nini kila aina ya jamii ina aina zake za hadithi. Hadithi ambazo zimekuwa zinatumika kufundisha maadili na misingi mbalimbali kwenye jamii hizo.
Sisi binadamu tunaelewa zaidi kupitia hadithi kuliko maelezo ya kawaida. Pia tunakumbuka zaidi hadithi kuliko tunavyoweza kukumbuka maelezo mengine tunayopewa.
Kupitia hadithi, tunauvaa uhusika, na kujiona moja kwa moja kwenye kile ambacho tunaelezwa.
Sasa unapaswa kutumia hadithi kwenye kile unachofanya.
Kama unataka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe, wakupe kazi au wanunue kile unachouza, tumia hadithi.
Hadithi zinashawishi na kuuza kuliko maelezo ya kawaida.
Lakini kuna kitu muhimu unapaswa kujua hadithi, haipaswi kuwa kuhusu wewe, bali inapaswa kumlenga msikilizaji.
Mpe msikilizaji hadithi ambayo atakuwa tayari kuwashirikisha wengine,
Hadithi ambayo ni rahisi kwake kuikumbuka na vigumu kuisahau.
Hadithi ambayo inampa msikilizaji taswira ya vitu kuwa bora kuliko vilivyo sasa.
Tengeneza hadithi ambazo ni kweli na zitumie hizo kuelimisha, kushawishi na kuuza.
Usijiambie wewe siyo mtu wa hadithi, hakuna aliyezaliwa akiwa mtu wa hadithi, ni kitu ambacho watu huwa wanajifunza.
Kama upo makini na kile unachofanya, basi wekeza muda wako kujifunza kuhusu hadithi na kutengeneza hadithi zitakazokusaidia kuwafikia wengi zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante kocha kwa ujumbe huu , kweli kupitia hadithi watu uelewa zaidi , Nitajifunza namna ya kuwa mtunzi wa hadithi
LikeLike
Vizuri James.
LikeLike