“The further any purpose the faster we should work toward it.” —GIUSEPPE MAZZINI

Kadiri kusudi la maisha yako linavyozidi kuwa kubwa, ndivyo unavyopaswa kuchukua hatua kubwa na za haraka.
Tofauti na hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe.
Huwezi kuwa na kusudi na malengo makubwa, halafu ukachukua hatua za kawaida na ukategemea kufikia kusudi na malengo hayo.
Utakuwa unajidanganya kama siyo kuwachekesha wengine.
Malengo au mpango wowote mkubwa ulionao kwenye maisha yako,
Kwanza waangalie wale ambao tayari wameshafika pale unapotaka kufika,
Kisha angalia ni vitu gani huwa wanafanya na vitu gani huwa hawafanyi.
Kisha ishi maisha ya aina hiyo, fanya yale wanayofanya na epuka yake wasiyofanya.

Kila mtu anapenda kusoma hadithi za waliofanikiwa sana,
Kila mtu anayajua maisha ambayo waliofanikiwa wamekuwa wakiyaishi.
Lakini inapofika kwenye kuishi kwa namna hiyo, wengi huona ni mateso, kutokujijali na kutokuyafurahia maisha.
Hivyo wanajifanya wanajua sana kuliko hao waliofanikiwa, kwamba wanaweza kufanya kawaida, kuishi kama wengine wa kawaida wanavyoishi halafu wapate mafanikio makubwa.
Hivi ndivyo wengi wanavyojidanganya na kujizuia kufanikiwa.

Huwezi kujiambia unataka kuwa bilionea, halafu unalala muda mrefu, unabishana kwenye kila aina ya ubishi, unafuatilia kila aina ya habari ba maisha ya wengine, unanunua vitu ili uonekane na wengine, unatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii na una muda mwingi wa kukaa na wengine kupiga soga na mapumziko ya kila siku ya kujiburudisha.
Haiwezi kutokea, unaweza kujidanganya utakavyo, lakini usije kulalamika pale maisha yako yanapokwama na kugoma kupiga hatua.

Malengo makuwa yanahitaji hatua kubwa na za haraka,
Anza mapema kuchukua hatua hizo, na zichukue bila kukosa.
Unafikiri kwa nini ni wachache kwenye jamii waliopiga hatua kubwa?
Kwa sababu ni wachache walio tayari kulipa gharama inayohitajika ili kufanikiwa.
Kama wewe ni mmoja wa hao wachache, weka sababu chini sasa na anza kuishi kwa misingi sahihi ya kukufisha unakotaka kufika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania