Rafiki yangu mpendwa,

Kila mmoja wetu kuna mambo anapenda sana kufanya kwenye maisha yake, lakini anakwamba.

Na moja ya vitu vinavyomwamisha kila mtu ni muda.

Mambo ni mengi na muda ni mchache, hii ni kauli ambayo imepata umaarufu mkubwa kwenye zama tunazoishi sasa.

Mambo ya kufanya, yale yanayotaka muda na umakini wetu yanazidi kuongezeka kila siku, lakini muda tulionao ni ule ule.

Hili limekuwa chanzo cha msongo kwa wengi, kwa kutaka kujaribu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Kwa kuona tatizo hili ambalo linawasumbua wengi, mimi rafiki yako niliamua kutafuta suluhisho ambalo litatusaidia wote.

Katika kutafuta suluhisho hilo, ndipo niliandika kitabu kinachoitwa PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

MASAA MAWILI YA ZIADA

Nilipoandika na kuanza kutoa kitabu hiki, kuna watu kabla hata hawajakisoma walikuwa wanasema huwezi kupata masaa ya ziada kwenye siku, kila siku ina masaa 24.

Lakini kama watu hawa wangechukua hatua ya kusoma kitabu hiki, wangejionea wenyewe jinsi ambavyo wangeweza kupata muda wa ziada kwenye siku zao.

Sasa rafiki yangu, nakuja kwako kukuambia kwamba yale yote ambayo umekuwa unapanga kufanya lakini unajiambia huna muda, dawa ya muda ipo.

Je umekuwa unapenda kuandika lakini unajiambia huna muda?

Je umeajiriwa na unataka kuanzisha biashara ya pembeni lakini kikwazo ni muda?

Je una biashara na unataka kuitanua zaidi lakini unakwama kwa sababu ya muda?

Je unapenda kusoma vitabu ili uweze kujiboresha zaidi lakini muda ni kikwazo?

Kama umesema ndiyo kwenye swali lolote hapo juu, basi unahitaji hasa kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA.

Kitabu hiki kinakuonesha kwa mifano, jinsi unavyoweza kupata muda zaidi kwenye siku yako. Na kama ukiweza kuwekeza muda huo vizuri, utakuwezesha kufanya makubwa na kupiga hatua kubwa zaidi.

Utajionea mwenyewe ni maeneo yapi yanayochukua muda wako mwingi na hayana mchango mkubwa.

Utajifunza jinsi ya kujiwekea vipaumbele ili kuzia yale yasiyo muhimu yasivamie siku yako na kula muda wako.

Kwa kifupi nikuambie tu rafiki yangu, kitabu PATA MASAA MAWILI YA ZIADA ndiyo mwarobaini wa tatizo la muda ambalo kila mmoja wetu anapitia kwa sasa.

Jinsi ya kupata kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA.

Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 5 (5,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 3 (3,000/=)

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 3 (3,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha PATA MASAA MAWILI na utatumiwa kitabu hicho.

Mwanafalsafa Seneca amewahi kusema, tatizo la muda siyo kwamba tunao mchache na hautoshi, bali tunao mwingi mpaka tunauchezea na kuupoteza. Kitabu cha PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU kitakuonesha jinsi unavyochezea na kupoteza muda wako na kisha kukuonesha jinsi ya kuuokoa na kuutumia vizuri kwa manufaa yako. Pata nakala yako ya kitabu hiki leo.

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
  2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
  3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
  6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
  7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
  8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania