Seneca said, “Hold fast, then, to this sound and wholesome rule of life…The body should be treated more rigorously, that it may not be disobedient to the mind.”
Ukiusikiliza sana mwili wako, hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Kwa asili mwili huwa haupendi kuchoka,
Hivyo unavyotaka kufanya kitu ambacho kitakuchosha, mwili utakuwa wa kwanza kulalamika.
Na hata ukivuka malalamiko hayo na kufanya, mwili utakuwekea vikwazo kwa kukupa maumivu makali.
Sasa hapo unakuwa ni mpambano wa mwili na akili.
Akili inataka ufanye au ufike sehemu fulani,
Lakini mwili haupo tayari kuweka kazi hiyo inayohitajika,
Hivyo utachoka na kuumia sana,
Hayo yote ni kukutaka usiendelee kuchukua hatua hizo zilizo ngumu.
Kama unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako,
Hatua ya kwanza ni kuufunza adabu mwili,
Kuufanya uisikilize akili inataka nini,
Na siyo akili kusikiliza mwili unataka nini.
Upe mwili mahitaji yake yote, chakula sahihi, mapumziko sahihi na kuulinda na hatari mbalimbali.
Lakini baada ya hapo, upe kazi sahihi ya kukufikisha kule unakotaka kufika.
Usiuonee mwili huruma, usiusikilize sana, utakupoteza.
Udhibiti mwili kwenye tamaa mbalimbali pia,
Kwa sababu akili ikiushinda mwili kwenye kuusukuka ufanye kazi,
Mwili unaleta mtego wa tamaa mbalimbali, kama ya ngono, vilevi, ulafi na kadhalika.
Hivyo lazima ujipange mapema kabisa kuzikataa tamaa hizo na kuhakikisha unapambana pale mwili unapokupeleka kwenye tamaa hizo.
Wakati mwingine unahitaji kuupitisha mwili kwenye magumu ili kuuimarisha, hasa unapokuwa umeshazoea ulegevu.
Kufunga kula au kunywa,
Kuunyima usingizi kwa siku kadhaa,
Kuupa baridi kali hata pale unapokuwa na njia ya kuupa joto,
Kuuweka kwenye mazoezi makali.
Na njia nyingine nyingi.
Hakuna ambaye amewahi kuusikiliza mwili na kukubaliana nao kwenye kila kitu akaweza kufanya makubwa.
Lazima uusukume sana mwili,
Wengine watakuambia unajitesa,
Lakini wewe unajua unataka nini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari,ukisoma kitabu cha Atlas Shrugged Cha Ayn Rand ndio utajua umuhimu na maana ya kutumia akili,mwili,moyo,hisia, hivi vikikuuongoza hakika utapotea Ila ukitumia akili na fikra sahihi utaweza kuniongoza hivyo na kufanya makubwa ktk maisha yako.
LikeLike