“If you want to be quiet and strong, work and improve your faith.” – Leo Tolstoy
Maisha hayajawahi kuwa nyoofu,
Japo unapanga nini unataka,
Na kuweka hatua za kuchukua ili kupata unachotaka,
Na kufanyia kazi hatua hizo kama unavyopaswa,
Siyo mara zote utapata unachotaka,
Na hapo ndipo jaribu kuu.
Wengi huishia kukata tamaa na kuona hakuna haja ya kuendelea kujisukuma na kujitesa, maana hawajapata walichotaka.
Lakini huo ndiyo wakati sahihi wa kuendelea,
Kwa sababu unakuwa na imani kwamba mambo yatakuwa mazuri mbeleni, japo kwa sasa huoni hilo.
Kama unataka kuwa tulivu na imara bila ya kusumbuliwa na chochote kinachoendelea, weka kazi kwenye kuboresha imani yako.
Amini kwenye mchakato, kwamba kwa kuchukua hatua sahihi, utapata matokeo sahihi, hata kama sasa huyapati.
Amini kwenye uwezo mkubwa uliopo ndani yako, kwamba haijalishi kwa sasa uko kwenye hatua gani, una uwezo wa kufanya makubwa zaidi.
Amini kwenye sheria za asili, kwamba kila thamani unayotoa lazima italipwa na hivyo endelea kutoa thamani zaidi, hata kama hulipwi kwa sasa, ni deni unalijenga kwa asili na lazima itakulipa.
Bila ya kuboresha imani yako, ni vigumu sana kuvuka magumu yaliyopo kwenye safari yetu ya mafanikio.
Na hili ni zoezi la kufanya kila siku na kila wakati,
Maana kuna nguvu kubwa inakazana kukukatisha tamaa na kukurudisha nyuma.
Lazima ujiamini sana, uamini mchakato na uiamini asili ili uweze kufanikiwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari, nitaendelea kujipambania ili kutoenda kinyume na Sheria za Asili,naona sheria za asilo zina maana kubwa sana ktk kuleta mabadiliko.
LikeLike