Kabla hujafikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, utashindwa mara nyingi sana.
Swali ambalo utakuwa nalo ni je watu wataendeleaje kukuamini ikiwa unashindwa?
Na jibu liko wazi, watu hawakuamini kwa kushinda au kushindwa kwako, bali watu wanakuamini kwa uadilifu ulionao.
Kama wewe ni mwadilifu, hata ushindwe mara ngapi, watu watakuamini, kwa sababu wanajua umefanya kile kilicho sahihi mara zote.
Lakini kama huna uadilifu, kushindwa mara moja ni tiketi ya watu kuachana na wewe kabisa.
Kwa sababu wanajua kukosa kwako uadilifu kumechangia kushindwa kwako, na hivyo hawategemei uje ufanikiwe baadaye kwa kukosa uadilifu.
Unaweza kusema dunia haina usawa, wakati kutokuwa na uadilifu kunakunufaisha, kuna watu watakuwa na wewe, lakini utakaposhindwa, watakukimbia kabisa.
Hapo ni swala la bahati tu, na watu wanajua bahati yako ikishapita hairudi tena.
Kama umepata mafanikio kwa kutokuwa mwadilifu, halafu mafanikio hayo yakapotea, hayawezi kurudi tena.
Lakini kama umepata mafanikio kwa kuwa mwadilifu na mafanikio hayo yakapotea, yatarudi tena, kama tu utaendelea kuwa mwadilifu na kufanya kile kilicho sahihi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Thanks
LikeLike