“Whatever happens, do not lose faith. Nothing bad can happen to you as a human being.” – Leo Tolstoy
Haijalishi nini kimetokea kwenye maisha yako, usipoteze imani.
Hakuna kitu chochote kibaya kinachoweza kutokea kwako kama binadamu.
Hakuna kitu kinachotokea ili kukuumiza au kukukomesha.
Kila kinachotokea, kinakuja kwako kwa lengo la;
👉🏼kukufundisha
👉🏼kukuimarisha/kukukomaza
👉🏼kukuamsha usingizini na uache mazoea.
Hivyo kila jambo unalokutana nalo kwenye maisha yako, jiulize limeleta nini.
Lakini hakikisha hupotezi imani kwa namna yoyote ile.
Maana ukishapoteza imani, unakuwa umeyakana maisha yako,
Na chochote kile kinaweza kukuangusha.
Ila unapoendelea kusimamia imani yako, kila kinachotokea kinakuja na manufaa kwako.
Kama bado uko hai, basi hakikishs imani yako iko imara.
Kwa sababu chochote kisichokuua, kinakufanya kuwa imara zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari hii hakika hii kwangu,nimeiona na ulyoyaandika hapo juu pia nimeyashuudia, japo huwezi kuyafanya,kuyaelewa kama hauko sehemu sahihi ya kujifunza.mara nyingi watu wanapotea tu pale wanapoanza kulaumu na kulalamika,wanapoteza muda mwingi kuliko kuanza kutafakari na kuchukua hatua sitaki.Mungu akubariki Sana kwa karama na kipawa hiki ulichojaliwa.
LikeLike
Vizuri sana Beatus,
Kila la kheri.
LikeLike