“The beginning of a quarrel is like a flood which breaks through a dam. As soon as it rushes through, you cannot stop it.” —The TALMUD

Kuanzisha ugomvi ni sawa na maji kuvunja bwawa, yakishatoka huwezi tena kuyazuia.
Kuanzisha ugomvi ni sawa na kuwasha moto msituni, ukishakolea huwezi tena kuuzima.
Epuka sana kuanzisha ugomvi, bila ya kujali umefanyiwa nini.
Gharama utakayoilipa kwa kuanzisha ugomvi, ni kubwa kuliko manufaa yoyote unayoweza kupata.
Epuka sana kuanzisha ugomvi,
Puuza sana mambo madogo madogo,
Na weka muda na nguvu zako kwenye mambo unayoweza kudhibiti na kuathiri moja kwa moja.
Kwa yaliyo nje ya uwezo wako, achana nayo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania