“Clever people study in order to know more. Undeserving people study to be more known.” —EASTERN WISDOM
Changamoto kubwa kwenye maisha ni kwamba watu wengi hawajifunzi ili kujua, bali wanajifunza ili kujulikana.
Mtu anaenda shule siyo ili apate maarifa yatakayobadili maisha yake, bali ajulikane na yeye ameenda shule au kufika kiwango fulani cha elimu.
Ndiyo maana tuna wengi waliosoma, lakini wachache mno walioelimika, ambao wametumia elimu waliyoipata kubadili maisha yao na kuwa bora zaidi.
Wemgine wengi wanasoma vitabu siyo kwa ajili ya kujua, bali kujulikana.
Hawasomi vitabu na kutumia maarifa yaliyo kwenye vitabu hivyo, bali wanasoma vitabu ili waweze kuwaambia wengine kwamba wamesoma kitabu fulani.
Wengine wanatafuta au kununua vitabu, lakini hawavisomi,
Kwa sababu ni rahisi kuwaambia wengine umesoma kitabu fulani kwa kuwa unacho, kuliko kuonesha wengine mabadiliko uliyoweza kufanya kwenye maisha yako kutokana na vitabu ulivyosoma.
Acha sasa kufanya vitu ili kuonekana na kujulikana,
Badala yake fanya vitu ili uwe bora zaidi leo kuliko ulivyokuwa jana.
Nenda shule kama elimu utakayoipata itakufanya kuwa mtu bora zaidi ya ulivyo sasa, na siyo kama itakupa cheo au mshahara zaidi.
Nunua na tafuta vitabu kama pia unaweza kutenga muda wa kuvisoma na ukivisoma utachagua kuchukua hatua ili maisha yako yawe bora, na siyo kutafuta na kununua vitabu ili uonekane umesoma.
Unaweza kudanganya wengine wengi,
Lakini huwezi kujidanganya wewe mwenyewe.
Hata kama wengine watahadaika na maigizo yako, ndani yako utajua ukweli,
Na huo utakuumiza na kukufanya ujidharau.
Jifunze ili kujua na siyo kujulikana.
Ukikazana kujua, utajulikana.
Ukikazana kujulikana, hutajua.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari na elimu adimu unayonipatia nitaendelea kuitumia vizuri katika kujiletea mabadiliko katika maisha yangu.
LikeLike