Hakuna yeyote mwenye uhakika ya kwamba kesho inakuwaje.
Hata watabiri ambao wamekuwa wanapatia mara nyingi, bado anachotabiri leo kuhusu kesho hakina uhakika wa asilimia 100.
Kuna vingi huenda vimetabiriwa huko nyuma na vikatokea, lakini kuhusu kesho, hakuna mwenye uhakika.
Lakini pia hata pale mambo tunayotabiri yatatokea yanapotokea, madhara yake huwa siyo makubwa kama tunavyofikiria. Huwa tunakuza sana madhara, iwe ni mazuri au mabaya. Lakini kitu kinapotokea, tunakipokea na maisha yanaendelea.
Najua unajua hili, lakini napenda leo tujikumbushe, maana ni rahisi kusahau. Ni rahisi kubebwa na hofu zako na kupata matumaini kutoka kwa watabiri mbalimbali.
Kitu pekee unachoweza kufanya leo kikawa na manufaa kwako kesho, ni kuishi siku ya leo kikamilifu. Hii itakufanya uwe na maandalizi bora ya kesho na kuweza kukabiliana na lolote linaloweza kutokea.
Pia jua chochote kinaweza kutokea kesho, hata kile ambacho hutegemei kitokee. Hivyo maandalizi unayofanya, yaweke nafasi ya usichotegemea kutokea, kutokea.
Na mwisho kabisa, huna haja ya kuteseka leo kwa ajili ya kesho, hata kama unategemea kesho itakuwa mbaya kiasi gani, wewe kazana kuiishi leo, kufanya kile unachopaswa kufanya leo, na kesho itakapokuja, ikabili kama inavyokuja.
Ifurahie leo, huku ukijiandaa kuipokea kesho na kuiishi kama inavyokuja.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Thankyou Dr
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante Sana Dr Aman kwa Elimu nzuri,ifurahie Leo huku ukijiandaa kuipokea kesho na kuiishi kama inavyokuja, hakika tunayosababu ya kuishi Leo vizuri kuliko kuhangaika na kesho.
LikeLike
Karibu Beatus
LikeLike
Asante kocha kwa maarifa haya hakika mungu azidi kukubariki
LikeLike