“The most common and the most widely used deceit is the wish to deceive not other people, but yourself. And this kind of life is the most harmful.” – Leo Tolstoy

“Let us be truthful. This is the mystery of rhetoric and virtue, this is the biggest mystery, this is the highest achievement in art and the major law of life.” — HENRI AMIEL

Uongo wa aina yoyote ile ni mbaya,
Lakini uongo wa kujidanganya wewe mwenyewe, ni mbaya zaidi.
Huu ni uongo wenye madhara makubwa sana kwako,
Maana unajipa upofu na kufanya vitu ambavyo baadaye vitakuumiza sana.
Unajidanganya mwenyewe pale unapojipa matumaini hewa,
Pale unapoacha kuweka juhudi na kutegemea mambo yatokee yenyewe,
Pale unapofunika tatizo ukifikiri litapotea,
Pale unapowaiga wengine ukifikiri utaonekana umefanikiwa,
Pale unapofuata kundi kubwa ambalo halipo sahihi na kuacha njia yako,
Pale unapojiambia utafanya kesho kile ulichokuwa umepanga kufanya leo.
Pale unapoamini kuna njia ya mkato ya kufanikiwa.
Pale unapoona waliofanikiwa kuliko wewe wamependelewa na wewe umenyimwa.
Pale unapojiambia huna cha kufanya,
Pale unapoamua kufanya kidogo kwa sababu unalipwa kidogo,
Pale unapotumia njia zisizokuwa sahihi kufanikiwa.
Zote hizo na nyingine nyingi ni njia ambazo umekuwa unatumia kujidanganya wewe mwenyewe.
Na kinachosikitisha ni kwamba, unaamini ni kweli kabisa, wakati unajua unajidanganya.

Unapaswa kuwa mkweli kwa watu wote na nyakati zote,
Lakini ni muhimu zaidi kuwa mkweli kwako wewe mwenyewe.
Kuwa mkweli hata kama ukweli huo unakuimiza,
Kwa sababu ukweli pekee ndiyo utakaokuweka huru.
Badala ya kujidanganya utafanya kesho kile ulichokuwa umepanga kufanya leo, jiambie ukweli kwamba hutakifanya kabisa. Na hapo ona ni madhara gani unatengeneza.
Badala ya kujiambia hujafanikiwa kwa sababu kuna nafasi umenyimwa au hujapewa, jiambie ukweli kwamba hujafanikiwa kwa sababu ya uzembe wako mwenyewe, halafu angalia namna gani ya kuondoka kwenye uzembe huo na kufanikiwa.

Uongo ni kama kilevi, kinakufanya usahau matatizo yako kwa muda lakini hakiyaondoi.
Na kilevi kinakuwa kibaya zaidi pale unapokuwa mteja na kukitegemea.
Kuna watu wameshajidanganya kiasi kwamba hawawezi kuishi tena bila ya uongo.
Na hiyo ndiyo hatari kubwa zaidi.

Ukabili ukweli, ishi ukweli mara zote.
Na utakuwa na maisha huru bila ya kujali nini unapitia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania