Haijalishi unapitia nini, kuna kitu cha kushukuru.
Unaposhukuru, unaangalia upande chanya wa maisha yako.
Na kwa kuwa akili zetu hutuonesha kile tunachofikiria,
Unapokuwa mtu wa shukrani, mambo mazuri zaidi yanakuja kwako.
Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto, kuwana kijitabu (diary) na kiite kitabu cha shukrani.
Kisha kila siku andika yale unayoshukuru kuwa nayo kwenye maisha yako.
Kila siku jilazimishe kuandika mambo, vitu au watu 3 unaoshukuru kuwa nao kwenye maisha yako, na kwa nini unashukuru.
Na utaona jinsi mtazamo wako kuhusu maisha utakavyobadilika.

Tunajifunza nguvu ya hili kutoka kwa Mstoa Marcus Aurelius, ambaye kwenye kitabu ambacho kilikuwa diary yake (meditation) ameanza kwa kutaja watu ambao anashukuru sana kuwa nao kwenye maisha yake.
Na sisi tuna mengi mno ya kushukuru, bila ya kujali tunapitia nini.
Kila siku kaa chini na andika yale unayoshukuru kwenye maisha yako na kwa hakika hutaweza kukata tamaa.
Muhimu; fanya zoezi hili kila siku kwa kuandika kwa mkono wako mwenyewe. Kuna nguvu kubwa sana unapoandika, kuliko kufikiria tu.
Kocha.