A wise man was asked, “Is there a single word which you can follow throughout all your life?” And the wise man answered, “There is such a word. This is shu.” And the meaning of this word is, “If we do not want certain things to be done to us, we should not do such things to others.” —CHINESE WISDOM
Ipo kanuni moja ambayo huwa haishindwi,
Ukiweza kuiishi kanuni hii, maisha yako yatakuwa tulivu na yenye amani.
Kwa kuishi kanuni hii utaepuka magomvi na mikwaruzano isiyo na msingi.
Kanuni hii ni sheria ya dhahabu (golden law),
Ambayo inasema; watendee wengine kile ambacho ungependa kutendewa.
Au kwa upande mwingine; kama kuna kitu hupendi kutendewa, basi pia usiwatendee wengine kitu hicho.
Ni kanuni rahisi na inayoeleweka,
Haihitaji elimu kubwa kuweza kuiishi,
Bali inahitaji ustaarabu,
Na unyenyekevu wa kuweza kujiweka kwenye viatu vya wengine.
Usiwafanyie wengine kile ambacho hupendi kufanyiwa.
Kabla hujafanya chochote jiulize je kama wengine wangekufanyia wewe ungefurahi?
Kama jibu ni hapana basi usifanye,
Haijalishi unajishawishi kiasi gani kwamba ni sahihi kufanya.
Kumbuka sisi binadamu ni kitu kimoja,
Chochote unachofanya kuwadhuru au kuwaumiza wengine,
Unajidhuru au kujiumiza mwenyewe pia.
Unapoishi kwa kuwajali wengine, unakuwa umejijali mwenyewe pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari hii ya Asubuhi hakika isilopenda kitendewa ni vizuri usiwatendee wengine huo ndio upendo wa kweli.tutoe thamani kubwa kwa wengine.
LikeLike