Kuna vitu vitatu ambavyo vimekuwa vinawachochea watu kuwa na tabia ya wizi. Hata wale ambao siyo wezi, hubadilika na kuwa na tabia hiyo pale vitu hivyo vitatu vinapokuwepo. Kwa kujua vitu hivi vitatu na kuvifanyia kazi, itakusaidia kuondoa au kukomesha tabia ya wizi kwenye eneo lolote lile.
Kichocheo cha kwanza ni urahisi wa kuiba. Sisi binadamu huwa tunapenda kufanya kitu ambacho ni rahisi kwetu kufanya. Kadhalika kwenye wizi, wengi huiba pale inapokuwa rahisi kwao kufanya hivyo. Kama eneo lina mianya inayofanya wizi uwe rahisi, basi watu wataitumia mianya hiyo. Hivyo kuzuia au kukomesha wizi, fanya kuiba kuwe kugumu, watu hawapendi vitu vigumu.
Kichocheo cha pili ni ugumu wa kukamatwa. adha ya kuiba ni kukamatwa ukiwa unaiba au kuwepo kwa ushahidi kwamba umeiba, inapokuwa vigumu kukamatwa au ushahidi kupatikana, wengi huiba. Kwa kuwa hakuna namna wanaweza kukamatwa au kudhibitika kwamba wameiba, wengi watatumia nafasi hiyo kuiba. Hivyo kama unataka kuzuia au kukomesha wizi, fanya iwe rahisi kwa mwizi kukamatwa au ushahidi uwe wazi, kukamatwa inapokuwa rahisi, wengi huacha kuiba.
Kichocheo cha tatu ni mazoea. Kama watu wamezoea kuiba, wataendelea kufanya hivyo. Itafika mahali na wataona ni kitu cha kawaida kwao na wanaweza kabisa kugombana na yule anayewataka waache tabia hiyo. Kichocheo hiki cha tatu ni kigumu kukabiliana nacho, kwa sababu mazoea ni magumu kuvunja. Lakini ukifanyia kazi vichocheo hivyo viwili hapo juu, watu wanaacha tabia ya wizi. Na wakishaacha, hakikisha wanapoanza unakomesha mapema kabla haijawa mazoea.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante kocha.
LikeLike
Ni kweli Kabisa,
watu wanaiba kwa sababu zifuatavyo;-
1. Ni rahisi kuiba
2. Sio rahisi wao kukamatwa au kuonekana kwa ushahidi kwamba wameiba
3. Mazoea
Kwenye biashara yangu nitafanya kuiba kuwe kugumu, kukamatwa kuwe rahisi na kuwe na ushahidi ili kuepuka mazoea ya wizi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike