“Associate with people who are likely to improve you.” — Seneca
Watu pekee unaopaswa kujihusisha nao, ni wale ambao wanaweza kukufanya uwe bora kuliko ulivyo sasa.
Hawa ndiyo watu wanaoongeza thamani kwenye maisha yako,
Watu ambao wanakupa nafasi ya kujifunza kitu kutoka kwao au kupata hamasa ya kupiga hatua zaidi.
Kwa kuwa watu wanaotaka muda wako ni wengi, huku muda wako ukiwa mchache sana,
Tumia kigezo hicho kuchagua watu gani utajaojihusisha nao.
Unapaswa kuwa huru na maisha yako na kuchagua watu gani unataka kuwapa muda wako.
Hulazimiki kumpa kila mtu muda wako.
Kuna watu ukikaa nao unajisikia vizuri, unapata matumaini na hamasa ya kujisukuma zaidi.
Hawa ndiyo watu unaopaswa kuwa nao zaidi.
Lakini kuna watu ukikaa nao unajisikia vibaya, unakata tamaa na kuona mambo hayawezekani.
Hawa ndiyo watu wa kuwakwepa na kukataa kuwapa muda wako.
Kuwa makini sana kwenye hili na lisimamie vizuri,
Usitawanye muda wako kama vile ni kitu utakuwa nacho milele.
Bali kuwa nao bahili, kwa sababu unapoimaliza siku moja, maana yake ni una siku pungufu za kuwa hapa duniani.
Sasa kama unazipunguza siku hizo kwa watu wasio sahihi, ni sawa na kuchagua kuyapoteza maisha yako bure.
Jihusishe na watu wanaoweza kukufanya uwe bora zaidi,
Na siyo tu kwa kukusifia,
Bali kwa kukufundisha usichojua na kukuonesha ambacho hujafanya.
Kupitia wengine, una nafasi kubwa ya kuwa bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari,hilo najitahidi na hasa kitendo cha kuingia kisima cha Maarifa tayari napata marafiki sahihi wa kujifunza nao,na wengine inbox tumekuwa tunaongea na kushauriana pia,nafurahi kwa kujisukuma kuwa bora na mshindi wa kujifunza kila Siku katika maisha yangu,
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike