Rafiki yangu mpendwa,
Huenda umekuwa unasikia majina hayo matatu yakitajwa na wengi, hasa katika kupata maarifa na mwongozo wa mafanikio kwenye maisha yako.
Na huenda umekuwa unajiuliza tofauti ya watu hao ni wapi na je unamhitaji yupi katika hao watatu.
Tofauti kati ya watu hao zipo, tena kubwa tu na siyo unamhitaji nani kati yao, bali unawahitaji wote kwenye safari yako ya mafanikio.

Karibu leo ujue tofauti ya Mwalimu, Kocha na Menta na ujue jinsi ya kuwapata walio sahihi kwa mafanikio yako.
Mwalimu ni mtu ambaye anafundisha, huyu anazieleza dhana ambazo ni ngumu kwa njia rahisi kuelewa. Unapokuwa na mwalimu anakupa ufafanuzi wa mambo ambayo wewe peke yako inakuwa vigumu kuyaelewa. Mwalimu ni njia ya mkato ya kujifunza, kwa sababu anaweza kukuelezea kwa njia rahisi na ukaelewa kwa muda mfupi kitu ambacho ungepaswa kusoma kitabu cha kurasa 300 ndiyo uelewe. Mwalimu ni nyenzo muhimu sana kwako katika kupata maarifa sahihi yatakayokuwezesha kufanya maamuzi sahihi. Katika zama tunazoishi sasa za mafuriko ya taarifa na maarifa, unahitaji sana kuwa na mwalimu atakayekuongoza kwenye maarifa sahihi kwako kupata.
Kocha ni mtu ambaye anakupa mwongozo wa hatua za kuchukua ili kupata matokeo unayopata, na anakusimamia katika kuchukua hatua hizo. Tofauti na mwalimu ambaye anakufundisha na kuishia hapo, kocha anakwenda na wewe bega kwa bega mpaka kuhakikisha umepata kile unachotaka. Kocha ana ujuzi na mbinu mbalimbali pamoja na njia ya kuzisimamia ili mtu aweze kupata matokeo mazuri. Kocha ni mtu muhimu wa kukusimamia na kukufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha unapata unachotaka. Kwa kuwa nidhamu binafsi ni changamoto, unapaswa kuwa na kocha ambaye hatakubaliana na wewe kurahisi kuacha, na hivyo utajisukuma kufanikiwa.
Menta ni mtu ambaye ameshafika kule ambapo wewe unataka kufika, na hivyo anaweza kukushirikisha uzoefu wake katika safari aliyopita. Kupitia menta unajifunza njia sahihi za kuchukua na makosa ya kuepuka ili upate kile unachotaka. Menta anakusaidia usipoteze muda kujaribu mambo yasiyokuwa sahihi, kwani kupitia uzoefu wake atakuonesha kipi sahihi kufanya na kipi siyo sahihi. Katika zama hizi ambapo wengi wanajaribu mambo na kushindwa huku wakatishaji tamaa wakiwa ni wengi, unahitaji sana kuwa na menta, kwani atakupa uzoefu wake na pia utapata hamasa na msukumo, kama yeye ameweza basi hata wewe utaweza.
Karibu Upate Mwalimu, Kocha Na Menta Sehemu Moja.
Rafiki yangu mpendwa, kama ulivyojifunza umuhimu wa watu hao watatu, unawahitaji sana kwenye safari yako ya mafanikio. Unamhitaji mwalimu wa kukupa maarifa sahihi, unamhitaji kocha wa kukupa mwongozo na kukusimamia na unamhitaji menta wa kukupa uzoefu wake kwenye safari yako ya mafanikio.
Katika kuwachagua watu hao, lazima uwe na vigezo ambavyo unaviangalia.
Kwa upande wa mwalimu, kigezo kikuu ni awe anatoa maarifa yanayokusaidia kufikia malengo yako. Walimu wapo wa kila aina, kuchagua anayefundisha yanayopingana na malengo yako hataweza kukusaidia.
Kwa upande wa kocha, kigezo kikuu ni awe anaweza kujisimamia yeye mwenyewe. Unataka kocha ambaye hatakuonea huruma na kukubali sababu zako pale unapotaka kuacha ulichopanga kufanya. Na huyo lazima awe hajionei huruma yeye mwenyewe, ni wa kwanza kufanya kile anachokusimamia wewe ufanye.
Kwa upande wa menta, kigezo kikuu ni awe amefika kule ambapo wewe unataka kufika, kama unataka kufanikiwa kwenye biashara basi menta wako awe amefanikiwa kwenye biashara hiyo ndiyo aweze kukuonesha yeye alifanikiwaje ili iwe rahisi kwako kufanikiwa pia.
Rafiki yangu mpendwa, kwa bahati nzuri sana una nafasi ya kuwapata watu hao watatu kwa wakati mmoja kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuna walimu mbalimbali, ambao wanafundisha vizuri kwenye maeneo mengi. Kuanzia kwenye mafanikio, biashara, falsafa, mahusiano, uongozi na mengine. Unapokuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unapata maarifa sahihi ambayo ukiyafanyia kazi maisha yako yanakuwa bora sana.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kuwa chini ya mwongozo na usimamizi wa karibu wa kocha. Huishii tu kujifunza, bali pia unapaswa kutoa mrejesho wa hatua unazopiga kwenye maisha yako, kupitia taarifa za kujitathmini kila mwezi. Lakini pia unapotaka kufuatiliwa kwa ukaribu zaidi au unapokuwa umekwama na unahitaji kujinasua, basi unaye kocha wa kukusaidia kwenye hilo.
Muhimu zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuna mamenta ambao unaweza kujifunza mengi kwao, na wako tayari kukushirikisha yale wanayojua kupitia kile wanachofanya. Kuna wengi waliopiga hatua na wanaendelea kupiga hatua zaidi kwenye nyanja mbalimbali za maisha, kuanzia uandishi, biashara, taaluma, uongozi, falsafa na kadhalika. Hivyo chochote unachotaka kuwa, kuna watu wa kukupa uzoefu wao.
Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unajichelewesha kwenye safari yako ya mafanikio. Kwani nje ya KISIMA huwezi kujua kipi ujifunze, maana walimu ni wengi na maarifa yao yanakinzana, mwalimu A anakuambia fanya hiki huku mwalimu B anakuambia usifanye hicho. Unabaki njia panda usijue nini cha kufanya. Ndani ya KISIMA hutapata njia panda hiyo, kwa kuwa walimu wote wanakufundisha kitu kimoja, njia sahihi kwako kupata mafanikio makubwa kwenye maisha.
Kadhalika kwenye KISIMA unampata kocha ambaye siyo tu anakusimamia wewe kufanikiwa, bali pia anajisimamia mwenyewe kufanikiwa. Unampata kocha ambaye mpo safari moja, kila siku anakazana kuwa bora zaidi na hapo mnakuwa pamoja kwenye safari ya mafanikio.
Muhimu zaidi ni unapokuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unakuwa umezungukwa na watu ambao wote mna uelekeo mmoja, wote mna kiu kubwa ya kufanikiwa na hivyo unapata msukumo mkubwa pamoja na kujifunza kupitia uzoefu wa wengine pia.
Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo, ili unufaike kuwa kwenye jamii ya kipekee na upate Mwalimu, Kocha na Menta watakaokusaidia kwenye safari yako ya mafanikio.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania