“Every thought a person dwells upon, whether he expresses it or not, either damages or improves his life.” —LUCY MALORY

Kila wazo unaloruhusu likae kwenye akili yako,
Lina madhara kwenye maisha yako,
Iwe utalifanyia kazi wazo hilo au la.
Madhara ya wazo yanategemea aina ya wazo lenyewe.
Kama wazo ni zuri linaleta madhara chanya, kwa maisha yako kuwa bora.
Na kama wazo ni baya linaleta madhara hasi kwa maieha yako kuwa hovyo.
Hakuna kitu chenye nguvu kubwa ya kuathiri maishs yetu kama mawazo tunayoruhusu yaingie kwenye akili zetu.
Wewe ni kile unachofikiri.

Pamoja na umuhimu na nguvu hii ya fikra zetu,
Bado tumekuwa hatuzipi uzito unaostahili.
Ukiwa nyumbani kwako na mtu akaja na uchafu na kuumwaga ndani kwako, hutaelewana naye.
Utapambana naye mpaka aondoe uchafu huo.
Lakini kila wakati unaruhusu watu wamwage uchafu kwenye akili yako,
Kwa kuwaruhusu wakupe habari hasi, wakujaze hofu na kukukatisha tamaa.
Yaani wewe mwenyewe unakazana kuutafuta uchafu wa kujaza kwenye akili yako, kwa kufuatilia habari mbalimbali na kuhakikisha huachwi nyuma na yale yanayoendelea, ambayo mengi hayana mchango wowote kwako.

Umefika wakati sahihi kwako kushika hatamu ya maisha yako.
Ni wakati wa kuweka mawazo sahihi kwenye akili yako, na kuondoa kila aina ya mawazo ambayo siyo sahihi.
Fanya usafi wa uhakika kwenye akili yako kwa kuondoa kila aina ya mawazo yasiyo sahihi.
Na weka ulinzi mkali kwenye akili yako kuhakikisha mawazo yasiyo sahihi hayaingii.

Wewe ni matokeo ya kile unachofikiri, hivyo hakikisha unafikiri kile kilicho sahihi.
Fikiri kile tu unachotaka kitokee kwenye maishs yako, na siyo vinginevyo.
Fikiri kile unachotaka kupata na siyo usichotaka kupata.
Maana akili yako inafanyia kazi kila wazo, haichagui hasi wala chanya.
Hivyo wewe ondoa hasi na baki na chanya.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania