Rafiki yangu mpendwa,
Kama hakuna mtu amewahi kukuambia au kusema kwa wengine kwamba una roho mbaya, ni kiashiria kwamba huwezi kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Kama hakuna mtu anayekuchukia bila sababu yoyote, yaani hujawahi kumfanyia chochote kibaya, lakini anakuchukia tu kwa jinsi unavyofanya mambo yako, basi jua hakuna makubwa unayofanya na hivyo huwezi kufanikiwa.
Kwenye jamii zetu, nidhamu ni roho mbaya na ubora ni kiherehere.

Pale unapokuwa na nidhamu binafsi kali na ambayo haina huruma watu watasema una roho mbaya. Kwa sababu kwenye jamii zetu, watu huwa wanahesabu roho nzuri ni pale mtu anapokubaliana na wengine kwa kila kitu.
Ukiwa na msimamo wako, na kuishi msimamo huo bila kuuvunja, wengi watasema una roho mbaya. Kwa sababu watakuja kwako wakitaka ufanye vitu fulani, lakini kwa msimamo wako hutakubali kuvifanya, na hapo watachukia.
Mfano kwenye fedha, kama umejiwekea nidhamu kwenye matumizi yako ya fedha, ambapo unafanya yale matumizi muhimu tu, ila anakuja mtu kwako akitaka umpe fedha, unapoanza kumhoji ina umuhimu gani au ameshafanya nini kwa kile anachopitia, hapo ataona hujali na una roho mbaya.
Pale unapojisukuma kufanya kwa ubora zaidi, pale unapokwenda hatua ya ziada kwenye chochote unachofanya, wale wanaokuzunguka ambao hawapo tayari kufanya kama wewe watasema una kiherehere, unajipendekeza au unataka uonekane zaidi.
Hii ipo sana maeneo ya kazi, kutokana na malengo yako ya kupiga hatua, unachagua kujituma kwenye kazi zako, wakati wenzako wanapiga majungu na kupoteza muda, wewe unaweka juhudi kwenye kazi. Haitachukua muda wewe ndiye utakayekuwa mada ya majungu, wataanza kukusema kwamba unakiherehere sana, unajipendekeza au kufanya ili wewe uonekane ni mzuri na wao ni wabaya.
Hata kwenye biashara pia, jaribu kuendesha biashara yako kwa namna yako mwenyewe, kwa kuachana na mazoea na kukazana kutoa thamani kubwa zaidi na wale wanaofanya biashara kama yako wataona unaharibu soko. Watakuona una kiherehere na kwa unayofanya unaharibu soko.
Huo ndiyo ugumu uliopo kwenye safari ya mafanikio, kwa kuwa umezungukwa na watu wengi ambao wanaishi maisha ya kawaida, pale utakapochagua kuishi maisha ya tofauti, unakuwa hatari kwao. Hivyo hawatakuacha salama, watahakikisha wanakushambulia mpaka uachane na mpango wako na kurudi kwenye maisha ya kawaida kwao.
Naamini unaijua hadithi ya kaa, ukimweka kaa mmoja kwenye chupa na kuiacha wazi, hatokaa muda mrefu, atatoka. Lakini ukiweka kaa wawili kwenye chupa, hata usipoifunika, hawatatoka. Kwa sababu pale mmoja atakapokazana kupanda, kabla hajafika mbali, mwenzake anamvuta kurudi chini. Hivyo wanatumia nguvu nyingi kuzuiana wasitoke, kuliko ambavyo wangeweza kuungana na kutoka.
Mfano huu una uhalisia mkubwa sana kwenye maisha yetu, kadiri unavyozungukwa na watu ambao hawajafanikiwa, ndivyo inavyokuwa vigumu sana kwako kufanikiwa. Kwa sababu kila hatua ndogo utakayopiga ya kuelekea kwenye mafanikio, watakazana kukuvuta urudi pale wao walipo, badala ya kuungana na wewe.
Na njia rahisi ya wanaokuzunguka kukuzuia usifanikiwe ni maneno wanayotumia kwako, maneno kama una roho mbaya, una kiherehere na mengineyo ni silaha kuu waliyonayo kuhakikisha hakuna anayeondoka kwenye kundi lao.
Mafanikio yanahitaji ngozi ngumu.
Kabla sijaijua misingi sahihi ya mafanikio nilikuwa nashangawa na jambo moja. Kila mtu ambaye amefanikiwa sana, huwa kuna maneno mabaya yanasema kwa ajili yake, wengine wanasemwa wameua watu wao wa karibu ili kufanikiwa, wengine wanasemwa hawajali, wana roho mbaya na maneno mengi ya aina hiyo.
Kilichokuwa kinanishangaza ni ukimya wa watu hao katika tuhuma hizo, wale waliofanikiwa sana hawakuwa na muda wa kujibu au kufafanua kwa wengine kwa nini hayo yanayosemwa siyo sahihi. Bali wao walikazana kuendelea kufanya mambo yao.
Nilikuwa nafikiri watu hao wanapaswa kutoa ufafanuzi kwenye yale wanayotuhumiwa nayo. Ni mpaka nilipojifunza misingi sahihi ya mafanikio ndiyo nikagundua kwamba wale waliofanikiwa zaidi, siyo tu hawaumizwi na mabaya wanayosingiziwa, bali pia wanayafurahia.
Huwa hawajitetei wala kutoa ufafanuzi kwa yale ambayo watu wanawatuhumu nayo, kwa sababu wakifanya hivyo, watakaribisha mabishano na tuhuma zaidi. Hivyo watu wakishachagua kuwapa tuhuma fulani, wanafurahia na kuacha tuhuma hizo ziendelee kuwepo, kwa sababu zinawapa watu kitu cha kuhangaika nacho huku hali hiyo ikimpa aliyefanikiwa uwanja wa kufanya yake.
Mfano watu wakishakuita una roho mbaya, kuna vitu vingi wataacha kukusumbua navyo, hivyo utakuwa huru kufanya mambo yako. Utakuwa tayari kusema HAPANA kwa kile ambacho hukubaliani nacho na watu watasema hata hivyo ana roho mbaya. Lakini wanapokukubali una roho nzuri, hata kama kitu hukitaki, itabidi useme tu ndiyo, maana ukisema hapana watakuambia, tulijua una roho nzuri na hutakataa hili.
Kama unataka kufanikiwa na kuishi maisha yenye uhuru kwako, unahitaji ngozi ngumu ya kuweza kukabiliana na mengi ambayo wale wasiofanikiwa watayaleta kwako.
Kwenye maisha ya mafanikio, roho mbaya ni tiketi ya wewe kuwa huru, kusimamia kilicho muhimu kwako na kuishi unavyotaka. Huku roho nzuri ikiwa gereza kwako, ikitumika kukufunga na kukuzuia kusimamia unachotaka.
Karibu Upate Ngozi Ngumu Ya Kubeba Mafanikio Yako.
Rafiki yangu mpendwa, kama tulivyojifunza hapo juu, bila ngozi ngumu huwezi kufanikiwa. Kadiri unavyozungukwa na wengi ambao hawajafanikiwa, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwako kufanikiwa. Maana wakiungana kwa umoja wao kukupiga vita, watakushinda kwa urahisi sana.
Unahitaji kuwa sehemu ya wale ambao wameshajitoa kupata mafanikio makubwa, ambao wameshatengeneza ngozi ngumu na isiyoumizwa na chochote. Hawa watakupa moyo wa wewe kuendelea na mapambano mpaka ufanikiwe.
Ipo sehemu moja ambapo unaweza kukutana na jamii ya aina hii, jamii ya watu wanaotaka mafanikio makubwa na ambao wanajijengea ngozi ngumu ya kubeba mafanikio hayo.
Sehemu hiyo ni kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kama unataka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, na kudumu kwenye mafanikio hayo, unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapata mafunzo sahihi na misingi pamoja na misimamo ya kuendesha maisha yako, ambayo haitetereshwi na yeyote. Utapata nguvu na ujasiri wa kusimamia kile kilicho sahihi kwako. Na hakuna hofu yoyote itakayoweza kukuteteresha na kukuondoa kwenye njia yako ya mafanikio.
Kama kweli umejitoa kufanikiwa, sehemu pekee ya kuwa ni kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Nje ya hapo, utakuwa laini sana kiasi kwamba maneno ya wengi yatakuumiza na kuona bora uungane nao kuliko kuendelea na safari ya mafanikio peke yako.
Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo, ili unufaike kuwa kwenye jamii ya kipekee kabisa, jamii ambayo ina ngozi ngumu ambayo haiwezi kusumbuliwa na maneno ya wale ambao wameshakata tamaa. Jamii ambayo maneno kama roho mbaya, kiherehere, kutojali, bahili na mengineyo ni kitu cha kawaida ambacho hakimstui yeyote.
Tena ukiwa kwenye jamii hiyo ya KISIMA CHA MAARIFA, unakaribisha kabisa maneno mabaya ya wengine na pale ambapo hawakuongelei vibaya, unajua kuna tatizo mahali na huenda umeshaanza kuwa kama wao.
Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania