“Remember that you are more free if you change your opinion and follow those who have corrected your mistakes, than if you are stubborn about your mistakes.” — MARCUS AURELIUS

Kama watu wamekuonesha kile unachofanya siyo sahihi, ni vyema kubadili na kufanya kilicho sahihi badala ya kuendelea kung’ang’ana na kitu hicho kwa sababu tu ndiyo umezoea kufanya.
Misimamo ya kijinga ndiyo imekuwa kaburi la wengi.
Ni asili yetu binadamu kupenda kuonesha msimamo, kwa kuendelea kufanya kile tulichozoea kufanya.
Lakini huwezi kufanikiwa kwa njia hiyo,
Lazima kila mara ujikague na kujitathmini,
Kama kila unachofanya kina mchango wa kukufikisha kule unakokwenda.
Kama kuna watu wanapata matokeo tofauti na yale unayopata wewe, kuna kitu wanakifanya tofauti na unavyofanya wewe.
Kujifunza kile wanachofanya na jinsi wanavyokifanya mpaka wakapata matokeo tofauti kisha na wewe kufanya hakukupunguzii chochote.
Badala yake kunakusaidia usiendelee kupotea.

Lakini hivyo sivyo wengi tunavyofanya,
Hasa tunapokuwa tumekosea,
Huwa hatukiri mara moja makosa yetu na kuyarekebisha ili kufanya kilicho sahihi.
Badala yake tunatafuta njia ya kuyahalalisha,
Tunatafuta sababu za kuturidhisha kwa nini imebidi tufanye tulichofanya.
Japokuwa sababu hizo zinaweza kuturidhisha,
Lakini je zinatusaidia nini?

Rafiki, njia ya kweli huwa ni moja pekee, lakini njia za uongo huwa ni nyingi mno.
Unaweza kuchagua kuhangaika na njia nyingi za uongo,
Au ukaitafuta moja ya kweli na kutumia hiyo.
Maisha ni yako na uchaguzi ni wako,
Kujidanganya ni rahisi, hilo ndiyo eneo la kwanza unalopaswa kulisimamia haswa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania