Andre Poisson alikuwa mfanyabiashara wa vyuma chakavu katika jiji la Paris nchini Ufaransa. Alikuwa na ndoto za kufikia mafanikio makubwa kibiashara na kuwa mmoja wa matajiri wa jiji la Paris hivyo alitafuta kila aina ya njia ya kufikia lengo lake.

Mwaka 1925 alikutana na fursa ambayo ingemwezesha kufikia lengo lake hilo la muda mrefu. Alipata taarifa ya siri kwamba mnara mkubwa uliopo Paris (Eiffel Tower) unauzwa kama chuma chakavu kutokana na serikali kushindwa kuufanyia marekebisho kwa kuwa gharama zake ni kubwa.

Andre Poisson hakutaka kupoteza fursa hiyo, aliifanyia kazi mara moja ili aweze kufikia lengo lake na hivyo alilipia ili kununua mnara huo akijua atapata faida kubwa itakayomfikisha kwenye utajiri mkubwa.

Lakini baadaye aligundua kwamba alikuwa ametapeliwa, mnara huo ulikuwa hauuzwi na aliyemtapeli alikuwa tapeli maarufu aliyejulikana kama Victor Lustig.

Lustig alikuwa tapeli maarufu wa miaka hiyo, ambaye alizunguka mataifa mbalimbali ya Ulaya na Amerika akitafuta watu anaoweza kuwatapeli. Mwaka 1925 akiwa mjini Paris alisoma makala kwenye gazeti ikieleza jinsi ilivyo gharama kutunza mnara maarufu wa mji huo unaoitwa Eiffel Tower. Maoni ya watu wengi ilikuwa ni mnara huo ubomolewe kuliko kuipa serikali gharama kubwa za kuutunza.

Na hapo ndipo Lustig alipoiona fursa ya kufanya utapeli, aliona nafasi ya kuuza mnara huo kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu.

Ili kukamilisha utapeli huo, Lustig alijipa cheo cha cheo cha serikali na kisha kutoa tangazo la siri kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu akiwaeleza nia ya kuuza mnara huo ili kupunguza gharama. Lakini ili kuzuia taharuki, serikali haitaki kuweka wazi kwamba inauza mnara huo, hivyo ni fursa kwa atakayeweza kuichangamkia.

Barua za kusudio la kuuzwa kwa mnara huo zilitumwa kwa makampuni matano yanayofanya biashara ya vyuma chakavu na wote walialikwa kukutana na Lustig ambaye alipanga mkutano kwenye hoteli kubwa ya kifahari. Mazungumzo yalikuwa ni ya siri na kila aliyepata nafasi ya kukutana naye alioneshwa jinsi hiyo ilivyo fursa kubwa na asipochukua hatua haraka ataikosa.

Katika mikutano hiyo Lustig alieleza kile ambacho kilikuwa kinasemwa sana kuhusu mnara huo, kwamba ni gharama kuuendesha na umma unaona ni bora uvunjwe kuliko kuendelea kuwa gharama. Kujenga imani zaidi alienda na wateja hao walengwa kutembelea mnara kwa ajili ya kuukagua na hapo aliwabeba kwenye gari la kifahari.

Baada ya kukutana na wafanyabiashara hao watano, Lustig alimchagua Andre Poisson kama mteja sahihi atakayeweza kunasa kwenye utapeli huo kwa sababu alikuwa na sifa zifuatazo; tamaa ya kufanikiwa haraka, kutokujiamini na fedha ya kuweza kununua mnara huo.

Mke wa Possion alipata wasiwasi na mkakati huo wa kibiashara na jinsi ulivyoendeshwa kwa siri na kwa haraka. Hilo lilimpelekea Possion kusita, kitu ambacho kilimfanya Lustig achukue hatua zaidi. Aliandaa mkutano mwingine wa siri na Possion akimweleza kwamba yeye ni mfanyakazi wa serikali ambaye anataka kumsaidia yeye anunue mnara huo kwa upendeleo na wengine wasipate nafasi hiyo, hivyo kama atampa rushwa, atamhakikishia hilo.

Kwa tamaa yake, Possion alimpa Lustig rushwa ili apate nafasi ya kununua mnara huo, na baadaye akalipia fedha kuununua. Hivyo akawa ametapeliwa fedha alizonunua nazo mnara huku pia akitapeliwa rushwa aliyotoa.

Hili ni tukio la kweli ambalo lilitokea kipindi hicho na haikuwa mara moja, kwani baadaye Lustig alipanga kuuza tena mnara huo kwa watu wengine, japo safari hiyo hakufanikiwa.

Utapeli umekuwepo tangu enzi na enzi, na mpaka sasa upo.

Kitu pekee kinachofanya utapeli uendelee kuwepo ni tamaa ya watu. Pale mtu anapokuwa na tamaa ya kupata mafanikio ya haraka, tena bila ya kufanya kazi ngumu, basi jua huyo ni mteja mzuri kwa matapeli.

Upo usemi ambao unasemekana kutolewa na aliyekuwa mwanamazingaumbwe maarufu P.T Barnum, usemi huo ni; kila dakika kuna mjinga mwenye tamaa anayezaliwa. Usemi huu una ukweli hasa unapoangalia jinsi watu wanavyoangukiwa kwenye utapeli ambao kwa akili ya kawaida tu unaweza kuona siyo kitu sahihi.

Unapokuwa na tamaa ya mafanikio, huku ukiwa hujui njia sahihi za kufikia mafanikio hayo, lazima utaishia kufanikiwa.

Kila wakati huwa inakuja michezo ya kitapeli, lakini tamaa za watu zinawazuia wasione ukweli. Miaka ya karibuni tumeona DECI, D9 na michezo mingine kama hiyo. Yote inakuja na jawabu la tamaa ya watu kupata utajiri bila ya kufanya kazi, kwamba unapanda pesa zako, na baadaye unakuja kuvuna, hakuna kupalilia wala kuweka mbolea, wewe panda, nenda nyumbani kalale kisha rudi siku ya mavuno. Kilichotokea kila mtu anajua, wengi wametapeliwa.

Kila siku utapeli mpya unakuja na ambao ni wa kijanja zaidi, kama hutakuwa mjanja, kama kutakuwa na misingi na misimamo sahihi, utaishia kutapeliwa kila wakati.

Karibu kwenye mazingira yatakayokuzuia usitapeliwe.

Rafiki yangu mpendwa, matapeli ni watu ambao wapo kazini. Kama wewe unavyofikiria jinsi gani utafanikiwa kwenye kile unachofanya, matapeli nao wanatumia muda wao wote kufikiria ni jinsi gani watakavyoweza kuwashawishi watu ili waweze kuwatapeli.

Hivyo kila wakati wanakuja na njia mpya na bora kabisa za utapeli, njia ambazo unaposikia kwa juu juu unakuwa na wasiwasi, ila ukiwapa nafasi na wakakueleza kwa kina, utaona safari hii ni tofauti, unashawishika, unaingia na unaliwa.

Ni vigumu sana kwako kuweza kuchambua kila aina ya utapeli na ukajua ni sahihi au siyo sahihi. Hivyo ni rahisi kwako kushawishika kwamba acha tu ujaribu, kwani hakuna mafanikio bila hatari, hivyo unajaribu kama hatari kwa kuwa kuna nafasi ya kufanikiwa. Baada ya kufanikiwa ndiyo unakuja kufunguka macho kwamba ulichojaribu siyo hatari, bali ujinga na tamaa.

Kuna mazingira ambayo yanaweza kukukinga wewe na aina yoyote ile ya utapeli, hata tapeli awe mjanja kiasi gani, hawezi kukupata ukiwa kwenye mazingira hayo. Mazingira hayo yanakujengea msingi na msimamo sahihi ambao hauwezi kutetereshwa na utapeli wa aina yoyote ile.

Mazingira hayo ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unaishi kwa msingi, mwongozo na msimamo sahihi wa mafanikio, hivyo ni vitu ambavyo unavitumia kufanya kila aina ya maamuzi yako, kitu ambacho kitakusaidia kuona wazi utapeli wowote unaoendelea.

Pia kwenye KISIMA, tunaishi kwenye msingi mkuu wa kazi, kwamba kazi ndiye rafiki wa kweli, kazi ndiyo njia pekee ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Tunaamini kwamba hakuna chochote halali na kinachodumu utakachoweza kukipata bila ya kuweka kazi ya wazi kabisa na inayoonekana na kila mtu. Tunaishi kwa falsafa hii; unaweza kupata chochote unachotaka kama utawapa wengine kile wanachotaka.

Kikubwa ni kwamba unapokuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unachagua lengo lako kuu unalifanyia kazi na eneo unalotaka kubobea, kisha unakomaa na vitu hivyo kwa angalau muongo mmoja (miaka 10) bila ya kuhangaika na vitu vingine. Unapochagua eneo moja na kukomaa nalo, hakuna anayeweza kukutapeli. Matapeli wanapenda wale ambao bado hawajachagua nini hasa wanataka na walio wazi kukimbilia kila aina ya fursa mpya.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajiweka kwenye hatari ya kutapeliwa na wale ambao ni wajanja na wanatumia udhaifu wetu binadamu kujinufaisha.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili uweze kuepuka matapeli wasinufaike na wewe, kwani ada utakayolipa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ni ndogo mno ukilinganisha na fedha na muda unaoendelea kupoteza kwa kukimbizana na kila fursa mpya unayosikia inalipa.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania