“One man keeps silence, and people discuss him. Another speaks a lot, and people discuss him. A third speaks a little, and people discuss him. There is no such thing as a person who is not being discussed or scolded.” — DHAMMAPADA
Kwa chochote unachofanya, watu watakuwa na cha kusema.
Wapo watakaosema kwa uzuri, wengine ubaya na wengine watakupuuza kabisa.
Tuchukue mfano kwenye kuongea,
Ukikaa kimja bila kuongea watu watakusema, wapo watakaosema una dharau, wengine watasema una aibu.
Ukiwa muongeaji sana bado watu watakusema, wapo watakaosema unajiona unajua sana, wapo watakaosema unaropoka.
Ukiwa muongeaji kiasi bado watu watakusema, wapo watakaosema unaringa na wengine watasema hujui.
Hivyo rafiki kama lengo lako kwenye kufanya kitu chochote ni kuwaridhisha watu wengine,
Tayari umeshindwa kabla hata ya kuanza kufanya.
Maana huwezi kuwaridhisha watu wote,
Hata ungekuwa nani.
Jukumu lako kuu kwenye maisha ni kuyaishi maisha yako,
Kwa namna ambayo yatakuwa bora kwako.
Ishi kusudi lako,
Fanya kile chenye tija kwako,
Na mara zote, angalia wale wanaoelewa unachofanya na nenda na hao.
Usijisumbue kufanya kitu ili kuwaridhisha watu wasikuseme.
Wala pia usihangaike kuwazuia watu kukusema,
Wewe fanya kazi yako, ambayo ni kuyaishi maisha yao.
Na waache wengine wafanye kazi yao, ambayo ni kuwasema wengine.
Mwisho wa siku kila mtu atavuna kile alichofanyia kazi.
Mara zote ishi maisha yako na jiamini.
Fanya kile kilicho sahihi,
Na usiumizwe na wale wanaokusema vibaya,
Hawakisemi wewe, bali wanajisema wenyewe kupitia wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania