Rafiki yangu mpendwa,

Najua kwa miaka mingi umekuwa unaweka malengo na mipango mikubwa ya kufikia kwenye maisha yako, ili uwe na mafanikio makubwa.

Na tena unajisukuma ili uweze kufanya yale uliyopanga kufanya.

Lakini huwezi kuyafanya kwa muda mrefu, unakutana na changamoto au vikwazo vinavyokufanya ushindwe kuendelea.

Lakini unapowaangalia wengine, unaona wakiendelea kufanyia kazi mipango yao bila ya kukwama kwa namna yoyote ile.

Unaanza kuamini kwamba wao wana bahati nzuri, hawakutani na vikwazo unavyokutana navyo wewe. Au wameanzia kwenye mazingira mazuri kuliko yako.

Kwa fikra za aina hii, unaamini njia yako ni ngumu na za wengine ni rahisi.

Kuamini huko ndiyo kosa kubwa unalofanya na linalokuzuia usifanikiwe.

Unaweza usielewe hili kwa haraka, twende kwa mfano ili tuelewane vizuri.

Chukua mfano kwamba unachopanga ni kuwa mwandishi mkubwa na mwenye mafanikio. Kufikia lengo hilo kuna vitu viwili unavyopaswa kufanya kila siku, kusoma na kuandika. Lazima usome sana, yaani kujifunza mengi, na pia kazima uandike, kila siku. Mengine yote unayofanya nje ya hayo mawili, ni nyongeza tu, lakini bila hayo mawili huwezi kufikia lengo kubwa ulilojiwekea.

Lakini sasa nini kinakwenda kutokea kwenye siku zako? Utapata muda wa kufanya mambo mengine yote, kasoro muda wa kusoma na kuandika. Utapata muda wa kula mara tatu, kuoga, kufuatilia habari, kuzurura mitandaoni, lakini muda wa kukaa chini usome au uandike, utakuwa mgumu mno kupatikana. Na hicho ndiyo kinakuwa kikwazo kikuu kwa mafanikio yako.

Kadhalika kwenye mambo mengine unayotaka kufanikiwa, iwe ni kwenye biashara, kazi au mambo mengine binafsi, kuna hatua fulani unapaswa kuchukua kila siku, ambazo haupo tayari kuzichukua kwa sababu mbalimbali na hicho ndiyo kinakuwa kikwazo kwako.

Inakuwaje ushindwe kuchukua hatua sahihi kwa mafanikio yako?

Rafiki, unaweza kujiuliza inawezekanaje ujue hatua sahihi za kuchukua lakini usizichukue?

Na hapo ndipo unapokwenda kumjua adui yako mkuu na anayekuzuia wewe usifanikiwe, maana ndiye anayekuzuia usichukue hatua unazopaswa kuchukua.

Adui huyo ni ubongo wako mwenyewe.

Unajua jinsi ambavyo ubongo wako ulivyo na nguvu na uwezo wa kufanya makubwa. Lakini pia ubongo huo ndiyo kikwazo cha kwanza kwako.

Iko hivi rafiki, ukubwa wa ubongo wako ni sawa na asilimia 2 ya mwili wako, kwa kulinganisha ni sehemu ndogo mno ya mwili wako.

Lakini katika matumizi ya nishati ya mwili, ubongo peke yake unatumia robo ya nishati yote inayozalishwa mwilini, hiki ni kiwango kikubwa mno.

Kiwango hiki kikubwa cha nishati kinachotumiwa na ubongo, huwa kinaenda kwenye kufikiri na kufanya maamuzi sahihi, hivyo inakuwa ni gharama kubwa kwa mwili wako.

Sasa kwa kuwa mwili unahitaji nishati kwa mambo mengine, ubongo umejifunza kupunguza matumizi yake ya nishati, kwa kuepuka kufikiri au kufanya maamuzi mengi.

Na hapo ndipo ubongo wako unapogeuka kuwa adui kwako, kwa sababu kila unapopanga kufikiri na kufanya maamuzi makubwa kwenye hatua unazochukua, ubongo unaahirisha, kwa sababu unajaribu kutunza nishati isipotee. Ndivyo ubongo ulivyo, unatunza nishati iwapo kutatokea hatari basi iwepo kwa kuuokoa mwili.

Unapousikiliza ubongo wako pale unapokuambua umechoka, au huwezi au utafanya wakati mwingine, unafikiri unakuambia ukweli, kumbe unakuhadaa tu. Ubongo huo unakupa sababu nyingi ili tu usifanye kitu kinachohitaji kutumia nguvu kubwa za mwili katika kufikiri.

Na hapo ndipo unaweza kupata mwanga kwa nini mtu akose muda wa kusoma au kuandika kwenye masaa yake 24 ya siku, lakini apate muda wa kufuatilia habari, mitandao ya kijamii na mengine yasiyo muhimu.

Ni kwa sababu mambo hayo hayahitaji nguvu kufikiria. Hivi umewahi kujikuta unaahirisha kufuatilia mitandao ya kijamii? Au umekaa mbele ya tv na kujiambia utaangalia baadaye au kesho? Jibu ni hapana, kwa mambo yasiyo magumu, ubongo haukupi kikwazo chochote, utafanya hata kwa masaa.

Lakini jaribu kufanya jambo gumu na muhimu, na hapo ubongo unabadilika haraka, unakataa usiendelee kutumia nguvu zake nyingi.

Unaweza kutumia simu hiyo uliyonayo kuzurura mitandaoni hata kwa masaa na isiwe shida yoyote kwako. Lakini kwa simu hiyo hiyo fungua kitabu na uanze kusoma ghafla usingizi mzito unakusonga, unaanza kusinzia. Naamini unaelewa usingizi huo unatoka wapi, ni ubongo unapinga usitumie nguvu nyingi za mwili.

Njia pekee ya kufanikiwa ni kuwa katili kwa ubongo wako.

Ukisikiliza ubongo wako, kamwe hutakuja kufanikiwa, kwa sababu ubongo unaamini kile unafanya kitu sahihi kwa kutunza nguvu za mwili, lakini nguvu siyo changamoto kwako.

Hivyo unachohitaji ili ufanikiwe ni kiwango fulani cha ukatili dhidi ya ubongo wako, kutokuusikiliza au kukubaliana nao kwa mambo mengi ambao unakupendekezea.

Ukishapanga kufanya kitu, fanya kama ulivyopanga, hata ubongo ukuambie nini, usiusikilize, wewe fanya kama ulivyopanga.

Unapojiambia huwezi kwa sababu huna muda au umechoka, panga muda na fanya. Usiruhusu ubongo wako ukimbilie kwenye jambo jingine lolote isipokuwa kufanya kile ulichopanga, kwa wakati uliopanga kufanya.

Kwa kuutumikisha ubongo wako namna hiyo, utaanza kufanya yale uliyopanga kufanya bila ya kuruhusu vikwazo au changamoto mbalimbali kukuzuia. Na hapo ndipo utaweza kufikia mafanikio makubwa, kwa kutoruhusu chochote kikurudishe nyuma.

Kwa kuangalia mahusiano yetu na ubongo, tunaweza kujumuisha vikwazo viwili vinavyotutenga na mafanikio tunayoyataka.

Moja ni huruma, kujionea huruma sisi wenyewe kumekuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio yetu.

Mbili ni kujidanganya bila kujua, kwa kujipa matumaini hewa tumekuwa tunatengana na mafanikio yetu.

Karibu kwenye mazingira yatakayokupa nguvu ya kuwajibisha ubongo wako.

Rafiki,

Unafikiri kwa nini wachezaji bora kabisa duniani wana makocha wanaowasimamia kwa karibu?

Unafikiri kwa nini mwanafunzi anapokuwa masomoni atafundishwa kila siku lakini hatapata msukumo wa kujisomea mpaka asikie kuna mtihani?

Unafikiri kwa nini tarehe ya mwisho kukamilisha kitu ndiyo watu wengi huchukua hatua?

Jibu la maswali hayo na mengine kama hayo unayoweza kuwa unajiuliza ni moja, peke yako huwezi. Hata uwe na malengo mazuri kiasi gani, hata uwe na msukumo mkubwa kiasi gani, peke yako huwezi kutekeleza.

Unashindwa kwa sababu unajionea huruma sana, haupo tayari kuwa katili kwa ubongo wako mwenyewe. Lakini pia ni rahisi sana kujidanganya wewe mwenyewe na kujiondoa kabisa kwenye yale sahihi kwako kufanikiwa.

Katika mazingira haya, unahitaji kuwa na mtu wa nje, mtu ambaye haangukii kwenye udhaifu wako wa ndani na hivyo anaweza kukusimamia kikamilifu ukamilishe kile unachopaswa kukamilisha.

Kama wachezaji wakubwa na ambao wameshashinda medani kubwa hawawezi kujisimamia wenyewe, unafikiri wewe ni nani uweze kujisimamia mwenyewe kufikia mafanikio makubwa?

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye mazingira ambayo ni sahihi kwako, mazingira ambayo yatakusimamia kwa karibu ili kuhakikisha hujidanganyi na badala yake unafikia mafanikio makubwa uliyojiwekea.

Mazingira hayo ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unaishi kwa msingi, mwongozo na msimamo sahihi wa mafanikio, hivyo ni vitu ambavyo unavitumia kufanya kila aina ya maamuzi yako, kitu ambacho kitakusaidia wewe kushinda kila aina ya ulaghai ambao ubongo wako utakuwa unakuletea.

Pia kwenye KISIMA, tunaishi kwenye msingi mkuu wa kazi, kwamba kazi ndiye rafiki wa kweli, kazi ndiyo njia pekee ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Tunaamini kwamba hakuna chochote halali na kinachodumu utakachoweza kukipata bila ya kuweka kazi ya wazi kabisa na inayoonekana na kila mtu. Tunaishi kwa falsafa hii; unaweza kupata chochote unachotaka kama utawapa wengine kile wanachotaka.

Kikubwa ni kwamba unapokuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unachagua lengo lako kuu unalifanyia kazi na eneo unalotaka kubobea, kisha unakomaa na vitu hivyo kwa angalau muongo mmoja (miaka 10) bila ya kuhangaika na vitu vingine. Unapochagua eneo moja na kukomaa nalo, hutapata nafasi ya kusikiliza uongo ambao ubongo wako unakuletea ili usiendelee kufanya kilicho kigumu na uende kwenye vitu rahisi.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kudanganywa na ubongo wako mwenyewe, kuendelea kupata muda wa kufanya kila kitu kwenye siku yako, kasoro vile unavyopaswa kufanya ili kufanikiwa.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili uweze kuwajibisha ubongo wako, ufanye kile unachopaswa kufanya na kuacha kukupa sababu zisizo na msingi.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania