Rafiki yangu mpendwa,

Siku za karibuni nimejiwekea udhibiti mkali mno kwenye ufuatiliaji wa habari za aina yoyote ile, hivyo mambo mengi yamekuwa yananipita, hasa habari mpya mpya, na hicho ni kitu kizuri kwangu.

Lakini zile habari ambazo zinawagusa wengi, nimekuwa nazipata kupitia mazungumzo ya wengine, au utani ambao watu wanakuwa wanaufanya kupitia habari hizo. Na hiyo ndiyo faida ya kutokusumbuka na habari, kwa sababu kama habari ni muhimu sana utaisikia kwa wengine, kama siyo muhimu itapotea yenyewe.

Moja ya habari ambayo ilipata bahati ya kunipita lakini nikaisikia kutoka kwa wengine ni kuhusu kupatikana kwa Bilionea mpya wa Kitanzania ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite. Mchimbaji huyo ameweza kupata kiwango kikubwa cha madini hayo ambacho kwa thamani yake inafikia shilingi za Kitanzania bilioni sana na.

Sina taarifa nyingi kuhusu mchimbaji huyo, kama alipataje madini hayo, amekuwa mchimbaji kwa muda gani na hata kiasi kamili cha fedha atakachokwenda kupata. Hivyo kwenye makala hii sitakuwa na sifa ya kumjadili au kumchambua mchimbaji huyo.

Lengo la makala hii ni kukujadili na kukuchambua wewe, kwa namna ambavyo unaweza kufikia ubilionea, bila ya kwenda kuchimba madini.

Moja ya vitu ambavyo huwa vinanifurahisha kuhusu Watanzania ni utani ambao huwa tunakuwa nao kwenye mambo mbalimbali.

Nakumbuka kipindi mchezaji wa Tanzania, Mbwana Samata alipoanza kucheza ligi kuu ya nchini Uingereza na mshahara wake kutangazwa ni milioni zaidi ya 600 kwa wiki, kila mtu alianza kusema anamfundisha mtoto wake mpira, ili aje apate pesa nyingi kama Samata.

Na kwa habari ya mchimbaji mdogo aliyepata ubilionea, nimeona watu wakiambiana waende wakachimbe madini ili nao wawe mabilionea.

Watu wanasema hayo kama utani, lakini kila utani huwa una ujumbe na ukweli ndani yake. Katika utani huu, inaonesha ni jinsi gani watu wanaamini ubilionea unapatikana kwenye vitu fulani fulani na siyo kwenye kile wanachofanya wao.

Ndiyo maana leo nimeona nikushirikishe makala hii inayokuambia kama lengo lako ni kuwa bilionea, usiende kuchimba madini, bali njoo ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA na fanyia kazi yale unayojifunza kila siku.

Kabla hatujaingia kuangalia jinsi gani KISIMA CHA MAARIFA kitakufikisha kwenye ubilionea, nijibu swali ambalo baadhi ya watu wameuliza, kama huyo mchimbaji mdogo ni bilionea. Jibu ni hapana, siyo bilionea, bali ni milionea wa namba moja (single digit millionaire). Thamani ya utajiri huwa inapimwa kwa sarafu moja inayoweza kuwa kiwango cha kupima watu wote, na kwa sasa sarafu inayotumika ni dola ya Marekani. Shilingi bilioni saba ni sawa na dola milioni tatu na za Kimarekani. Hivyo mchimbaji huyo ni milionea.

Jinsi kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kutakavyokufikisha kwenye ubilionea.

1. Mgodi wako uko hapo ulipo.

Nimewahi kukushirikisha hadithi ya bwana mmoja aliyeuza shamba lake ili kwenda kutafuta madini ya almasi, lakini alizunguka dunia nzima hakuyapata.  Mwishowe kwa uchovu na kukata tamaa, akajiua. Huku nyuma, yule aliyemuuzia shamba akiwa kwenye mfereji ulio kwenye shamba alilonunua anaona jiwe linalong’aa, anapolichukua na kufuatilia anakuta ni almasi. Kumbe shamba lile lilikuwa na almasi nyingi, lakini aliyeliuza hakujua hilo.

Hicho ndiyo kitu cha kwanza unachojifunza, kukiamini na kukiishi unapokuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwamba mgodi wako wa dhahabu, almasi au tanzanite uko ndani yako, uko hapo ulipo sasa, uko kwenye kile unachopenda kufanya, kile ambacho uko tayari kukifanya hata kama hakuna anayekulipa.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unajifunza kutafuta thamani pale ulipo sasa, kwenye kile unachofanya, kwa namna ambayo utaweza kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora na wao kuwa tayari kukulipa wewe. Utaacha kukimbizana na fursa mpya kila wakati na kuchagua ile fursa sahihi kwako na kuifanyia kazi.

2. Unahitaji muda kufikia ubilionea.

Kulala masikini na kuamka tajiri ni msamiati unaopatikana kwa masikini ambao huishia kufa masikini. Hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kufikia viwango vya juu vya mafanikio bila ya kuweka muda wa kutosha, hayupo na hatakuja kutokea. Hata ukimfuatilia mchimbaji aliyepata madini hayo, utaona hajaanza kuchimba leo, atakuwa na miaka mingi, zaidi hata ya 10 kwenye uchimbaji ndiyo akaja kupata manufaa aliyoyapata. Katika muda huo mwingi ambao amekuwa kwenye uchimbaji, kuna mengi aliyojifunza, ambayo yamemwezesha kupata nafasi aliyoipata.

Unapokuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, kiwango cha muda wa chini kabisa unaojiwekea ili kufanikiwa ni miaka 10 ya kuweka kazi hasa kabla hujapata mafanikio makubwa. Miaka angalau 10 ya kujituma, kuweka juhudi, kujifunza, kuwa bora zaidi.

Nje ya KISIMA CHA MAARIFA watu wanadanganyana sana, watu wanahangaika na fursa mpya kila wakati, ndani ya mwaka mmoja mtu anaanzisha na kuacha biashara 3 na zote anakuambia hazilipi, mwisho anakuambia nimejaribu kila kitu nimeshindwa.  Hapo unaweza kuona kwa nini watu hawafikii mafanikio makubwa, kwa sababu hawawekezi muda wa kutosha kwenye chochote wanachofanya.

Njoo kwenye KISIMA CHA MAARIFA uanze upya safari yako, ujipe miaka 10 mpaka 20 ya kufika mafanikio makubwa, ujifiche kwa miaka hiyo ukifanya kazi na kwa hakika lazima utafanikiwa kwa viwango unavyotaka.

3. Unahitaji ubobezi.

Mafanikio makubwa na hata ubilionea, vinahitaji ubobezi wa hali ya juu kwenye kile unachofanya na hata kwenye fedha pia. Hili ni jambo ambalo watu wamekuwa hawalipi uzito. Huwa wanafikiria tu kupata fedha nyingi, lakini angalia wengi waliopata fedha nyingi wameishia wapi. Wengi huishia kurudi kwenye umasikini waliokuwa nao, kwa sababu wanakimbilia kupata fedha kabla hawajapata ubobezi.

Fedha huwa zinakuja na kuondoka, lakini ujuzi na uzoefu mkubwa ambao mtu anakuwa amejijengea kwenye kile anachofanya huwa hauondoki, bali anabaki nao. Ukiangalia historia ya mabilionea wengi, kuna kipindi walipitia wakati mgumu, wakapoteza kila walichokuwa nacho, lakini baadaye wakarudisha kila walichopoteza, kwa sababu ubobezi wao haukupotea.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unachagua eneo ambalo unakwenda kubobea, kuwa bora kuliko watu wengine wote dunia nzima na kisha kuweka kazi kwenye kujenga ubobezi huo. Kwa kubobea, unakuwa huna wasiwasi, kwa sababu hata ukipoteza vitu ulivyopata, ubobezi wako utakuwezesha kuvirudisha vyote.

4. Ubilionea siyo fedha unazokuwa nazo, bali thamani ya uwekezaji wako.

Elon Musk ni mmiliki wa kampuni ya magari ya umeme (Tesla) na kampuni ya usafiri wa kwenda kwenye anga la nje ya dunia (SpaceX). Jarida la Forbes, ambalo kila mwaka limekuwa linatoa orodha ya matajiri duniani, mwaka 2020 linamtaja Elon kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 40.

Mwishoni mwa mwaka 2019 Elon alikuwa na kesi ambapo alikabiliwa na mashtaka ya kumkashifu mtu, ambapo angepaswa kulipa kiwango kikubwa cha faini. Wengi walijua kwa kuwa ni bilionea, basi ataweza kulipa faini hiyo bila shida. Lakini haikuwa hivyo, katika utetezi wake, Elon alisema japokuwa utajiri wake unathaminishwa kuwa na mabilioni ya dola, fedha halisi aliyonayo ni milioni chache sana. Utajiri wake umehesabiwa kwa hisa anazomiliki kwenye makampuni yake makubwa mawili na siyo kwamba hayo mabilioni ya dola anayo benki au nyumbani kwake.

Kwenye utetezi huo wa Elon tunajifunza kitu kikubwa sana kuhusu utajiri ambacho watu wengi wamekuwa hawakielewi. Ubilionea hauhesabiwi kwa fedha ulizonazo, bali kwa thamani nzima ya uwekezaji wako. Hivyo uzito unapaswa kuwa kwenye uwekezaji, na siyo kwenye kiasi cha fedha unachopokea.

Ninaweza kusema jambo moja kuhusu mchimbaji mdogo aliyepata mabilioni ya shilingi, kwamba maisha yake yanakwenda kuwa magumu kuliko yalivyokuwa awali. Kwa sababu hakuna kitu kigumu kama kukaa na fedha nyingi, na kigumu zaidi pale taifa zima linapojua una fedha nyingi. Utakuwa na ndugu wa kila aina, utapata washauri wa kila aina na kama haupo makini, utapoteza fedha karibu zote.

Ndiyo maana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, mkazo mkubwa upo kwenye uwekezaji, haijalishi unapokea kiasi gani, muhimu ni uwe na uwekezaji unaofanya, ambao baadaye utakuingizia wewe faida hata kama umelala.

Kama tulivyojifunza kwa Elon na hata kwa mabilionea wengine, huwi tajiri kwa kipato unachoingiza, bali kwa uwekezaji unaofanya, unaoongezeka thamani na kukuzalishia riba.

Njoo kwenye KISIMA CHA MAARIFA, uanze uwekezaji wako mapema, ili miaka 10 mpaka 20 ijayo, uweze kuingiza kipato hata ukiwa umelala.

5. Bahati pia inahusika.

Kwenye safari ya mafanikio, hasa kufikia mafanikio makubwa sana, bahati pia inahusika sana. kwenye jamii yoyote ile, ukiwachukua watu 100 na kupima mafanikio yao, kuna mmoja ambaye atakuwa na mafanikio makubwa kuliko mafanikio ya wale 99 waliobaki. Na hata kwa mchimbaji huyo mdogo, kuna wachimbaji wengine wengi ambao walianza uchimbaji kabla yake, lakini hawajawahi kupata alichopata yeye.

Sasa watu wanaposikia bahati, wanajiambia kila mtu ana bahati yake, au bahati ya mwingine usiilalie mlango wazi. Kitu ambacho wengi hawajifunzi ni kwamba bahati huwa inatengenezwa. Bahati inatokea pale fursa inapokutana na maandalizi. Kama unataka kukutana na bahati, unahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha kwenye eneo hilo, kisha kuwa na jicho la ziada la kuziona fursa kwenye eneo ulilochagua. Lazima uweze kuona kile ambacho wengine hawaoni ndiyo ufanikiwe zaidi.

Mmoja anayefanikiwa sana kuliko 99 wanaobaki, ni kwa sababu kuna kitu anaona ambacho wengine 99 hawakioni. Kwa nje tutasema ana bahati, lakini ndani yake ana maandalizi makubwa na anaziona fursa mapema kabla ya wengine.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unachagua eneo ambalo unataka kubobea, unajiwekea lengo kubwa unalotaka kufikia, kisha unaweka umakini wako wote kwenye vitu hivyo bila kuruhusu usumbufu wowote utawanye umakini wako. Utaanza kuona vitu ambavyo wengine hawaoni, utaweza kuchukua hatua na kupata matokeo makubwa, huku watu wakisema una bahati.

Rafiki yangu mpendwa, ninachoweza kukuambia ni kimoja, wewe unaweza kufikia mafanikio makubwa, wewe unaweza kubwa bilionea hasa (wa dola za kimarekani). Unachohitaji ni kuwa eneo sahihi, na eneo hilo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Usikimbilie kwenye kuchimba madini, huhitaji kubadili chochote hapo ulipo sasa, bali unachohitaji ni wewe kubadilika na dunia nzima itabadilika. KISIMA CHA MAARIFA ni eneo ambalo litakubadili, na kila siku litakusukuma uwe bora zaidi.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania