“People who watch you judge you on what you do, not how you feel.” – CUS D’AMATO
Watu wanaokuangalia huwa wanakuhukumu kwa kile unachofanya na siyo jinsi unavyojisikia.
Unachofanya kinaonekana na kila mtu,
Hisia zako unazijua mwenyewe.
Hivyo unapaswa kuwa makini, usiruhusu hisia zikusukume kufanya kile ambacho siyo sahihi.
Hata kama utajitetea kwamba ilikuwa hasira tu, lakini ulichofanya hakitafutika.
Kama unajijua ni mtu wa kusukumwa na hisia kufanya mambo, na baadaye unayajutia,
Basi jifunze kujizuia kukimbilia kuchukua hatua.
Kila wakati unapokuwa na hisia fulani, jipe muda kabla hujafanya maamuzi au kuchukua hatua yoyote ile.
Hisia huja na kuondoka,
Lakini kile unachofanya kitaendelea kuwa na wewe milele.
Kuwa makini sana na unachofanya, kitakuwa na wewe kwa muda mrefu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania