“People who want to write either do it or they don’t.” — Octavia Butler

Kama kuna kitu unataka kufanya, una machaguo mawili, kukifanya au kutokukifanya.
Chochote zaidi ya hayo mawili ni kujidanganya tu.
Kama unataka kuandika, unachagua kuandika au kutokuandika,
Kujiambia utaandika ukiwa na muda ni kujidanganya.
Kama unataka kuanzisha biashara ni utaanzisha au hutaanzisha,
Kujiambia utaanzisha ukiwa na muda au wazo au mtaji ni kujidanganya tu.
Mtu anayeamua kweli kufanya kitu, hakuna kinachoweza kumzuia asifanye.
Na mtu ambaye hataki kufanya kitu, ana sababu chungu mzima za kutokufanya, ambazo zitaonekana ni sahihi.
Hivyo usiwe mtu wa kujidanganya,
Watu wakikuuliza kwa nini hujafanya kitu fulani ulichosema utafanya,
Kabla hujakimbilia kwenye sababu za kujidanganya, waeleze wazi, sijafanya kwa sababu sijataka kufanya.
Maana kila mtu anajua, kama maisha yako yangetegemea wewe kufanya kitu hicho, kama ungeambiwa fanya au ufe, kwa hakika ungefanya.
Sasa ya nini kujifanganya na sababu zisizokuwepo?
Fanya au usifanye, usijidanganye na sababu zozote, hata kama zinaonekana ni sahihi.
Sababu hazileti matokeo yoyote,
Achana nazo mara moja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania