Rafiki yangu mpendwa,

Mwezi huu wa sita tunaoumaliza leo nimeutumia kukukumbusha kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa wale ambao bado hawajawa wanachama. Nimekukaribisha twende pamoja kwenye safari hii ya miaka kumi (2020 – 2030) ya kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.

Tunahitaji kupotea kwenye maisha ya kawaida kwa kipindi fulani ili kuweza kujenga mafanikio makubwa. Kwenye makala mbalimbali nilizokuandalia, nimekushirikisha mambo muhimu ya kuzingatia katika hilo.

semina 2017 4
Sehemu ya wahudhuriaji wa semina

Hivyo niendelee kukukaribisha sana, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi leo unayo nafasi ya mwisho ya kujiunga na uwe mwanachama, kwa kulipa ada yako ya mwaka. Na pia kama ni mwanachama na ada yako imeisha, ilipe kwa wakati ili tuendelee kuwa pamoja.

Kumekuwa na wasomaji ambao wameonesha nia ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ila hawawezi kumudu ada ya tsh laki moja (100,000/=) ambayo ni ada ya mwaka mzima kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Wapo ambao wameomba kulipa kidogo kidogo kwa kuwa hawawezi kulipa mara moja ada yote.

Kwenye makala ya leo naenda kushirikisha hatua unazoweza kuchukua kama huwezi kumudu ada ya KISIMA CHA MAARIFA.

 1. Kuhusu kulipa kwa awamu.

Mpango wa KISIMA CHA MAARIFA ni ulipe ada yako ya mwaka mara moja na uwe na mwaka mzima wa kujifunza bila ya kusumbuliwa. Kulipa kila mwezi tulishajaribu huko nyuma na ikawa ni usumbufu mkubwa, kila mwezi inabidi kutoa na kuingiza watu upya, kitu ambacho ni usumbufu kwa kila mtu.

Hivyo jitahidi uweze kulipa ada yote, na kama huwezi, basi kuna nafasi ya kulipa kwa awamu mbili ndani ya mwezi mmoja na ukamilishe ada yako. yaani ulipe elfu 50, uunganishwe kisha ndani ya mwezi mmoja umalizie elfu 50 iliyobaki.

 1. Jiunge na SOMA VITABU TANZANIA.

SOMA VITABU TANZANIA ni channel yenye vitabu na chambuzi za kina za vitabu mbalimbali. Channel hii inakupa mafunzo mengi sana kutoka vitabuni na hatua za kuchukua ili uweze kuyaboresha maisha yako.

Ada ya channel hii ni nafuu zaidi na unaweza kulipa kwa wiki, mwezi au mwaka. Kwa wiki ni elfu 1, kwa mwezi elfu 3 na kwa mwaka elfu 30.

Karibu ujiunge na channel hii kwa kufungua; https://www.t.me/somavitabutanzania

 1. Tembelea AMKA MTANZANIA kila siku.

Lengo la KISIMA CHA MAARIFA ni kutoa nafasi kwa wale ambao wameshajifunza bure kwenye mafunzo ninayotoa, yakawanufaisha na wanataka kupata zaidi. Hivyo kama huwezi kumudu kabisa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, usiumie, badala yake tembelea AMKA MTANZANIA (www.amkamtanzania.com) kila siku na usome makala nzuri sana zilizomo.

Ukishasoma makala hizo, fanyia kazi yale unayojifunza na utaanza kupiga hatua, kipato chako kitaongezeka, na hapo utaweza kumudu kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Huwa sishauri mtu ajiunge na KISIMA CHA MAARIFA kama hajajifunza bure na akanufaika na makala zilizopo kwenye AMKA MTANZANIA. Hivyo kama hujaweza kumudu ada ya KISIMA CHA MAARIFA, hakikufai, rudi kwanza kwenye AMKA MTANZANIA, soma makala, fanyia kazi na utapiga hatua, hapo sasa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA haitakuwa kazi ngumu kwako.

 1. Soma Vitabu Nilivyoandika.

Nimeandika vitabu mbalimbali, baadhi nakala ngumu na vingine nakala tete. Orodha ya vitabu hivyo iko hapo chini pamoja na bei zake na jinsi ya kuvipata. Chagua kitabu unachotaka, kipate, kisome, fanyia kazi na upate manufaa, kisha karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

VITABU VYA KOCHA DR MAKIRITA AMANI.

Hapa kuna orodha ya vitabu vyote vilivyoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Vitabu vinavyopatikana ni kama  ifuatavyo;

VITABU VYA SOFTCOPY (NAKALA TETE);

 1. Kwa nini mpaka sasa wewe siyo tajiri tsh elfu 5
 2. Jinsi ya kufaidika na mabadiliko yanayotokea tsh elfu 5
 3. Jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog tsh elfu 10
 4. Kurasa za maisha ya mafanikio tsh elfu 10.
 5. Biashara ndani ya ajira tsh elfu 10.
 6. Jinsi ya kupata masaa mawili ya ziada kila siku, tsh elfu 5.
 7. Ijue biashara ya mtandao (Network Marketing), tsh elfu 5.
 8. Mimi ni mshindi, ahadi yangu na nafsi yangu, tsh elfu 10.

Jinsi ya kupata vitabu vya softcopy; Tuma fedha na jina la kitabu unachotaka pamoja na email yako kwenye namba 0717396253 au 0755953887 kisha utatumiwa kitabu.

VITABU VYA HARDCOPY (NAKALA NGUMU)

 1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, tsh elfu 20.
 2. TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, tsh elfu 50.
 3. BIASHARA NDANI YA AJIRA, tsh elfu 20.

Kupata vitabu vya hardcopy piga simu au tuma ujumbe kwenda namba 0678 977 007 au 0752 977 170 na utapewa maelekezo ya kupata kitabu.

Kama ulikuwa hujapata taarifa za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA basi hapo chini ipo taarifa hiyo. Soma kisha karibia kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tuweze kusafiri pamoja kwenye mpango huu wa mafanikio makubwa.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

 1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
 2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
 3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
 4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
 5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
 6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
 7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
 8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
 9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
 10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania